HAKIKA SITOKUSAHAU.!!

MTUNZI;Dorcas Safiel.
SEHEMU YA NNE
.HAKIKA SITOKUSAHAU!!!
TULIPOISHIA;
Nancy kaanza sekondari na pia amejiunga na vikundi vibaya shuleni ili tu ajikizi na mahitaji yake baadhi

.TUENDELEE..Nikajiunga na kikundi kimoja pale shule ambayo kiukweli kila mtu alikuwa anajua kuwa kundi lile ni baya na ata hivyo walikuwa wamenipita kidato wao wakiwa ni kidato cha tatu,walimu na ata wanafunzi wenzangu walinisihi sana kutokuwa nao lakini kwakuwa wao walikuwa na mipango mingi ya hela na mimi ndo ilikuwa shida yangu nakumbuka mwenzi wa sita baada ya kufanya mitihani ya kufungia shule niliweza kupata ripoti yangu nakukuta kuwa nimefaulu vizuri..Mama yangu, na Dada zangu waliniambia kuwa nizidi kusonga mbele kitu chochote kisinirudishe nyuma kabisa nilihitika sawa na kunyanyuka na kuendelee na mambo mwingine.Kwa mwenzi huo ambao tulikuwa tu tuefunga shule nilikuwa tayari nimewakumbuka marafiki zangu nakumbuka mwenzi wa saba nilifungua shule na nikaitwa na mwalimu mkuu aliniambia kuwa nimefaulu sana lakini na bidii kuepukana na makundi mabaya niliyoaza nayo, nilimuitikia sawa nitaachana nao na aliiruhusu kuondoka baada ya maongezi kuishaMiaka kadhaa ilipita na mimi kuwa kidato cha tatu nilikuwa na mpenzi ambaye alininunulia simu na kuniambia kuwa itakuwa njia ya kuwasiliana naye wakati ambao niko naye mbali na nina shida ya kitu Fulani,nilikuwa naficha simu hiyo ili mama au kina dada wasijue na nilishukuru kwani nilikuwa nalala peke yangu nikaaza kuwa na mipango ya peke yangu kwakuamini kuwa naweza kufanya chochote kutokana na unzuri wangu na kujiamini mbele za watu wengi,nilidumu naye miezi kadhaa bila kukutana naye kimwili kuamini kuwa ni dhambi mbele ya mungu na maneno ya mama yalikuwa yanakuja na kutoka kichwani kwangu kuhusu kujitunza mwaka ukaisha na kuingia kidato cha nne lakini matokeo yangu hayakuwa manzuri maendeleo yalishuka kutokana na upendo niliokuwa nao sana wakuwa na Yule kaka ambaye siku nyingine nilikuwa siendi shule ili tu nikutane naye tukatembee huku na huko..Mama yangu kwa kipindi hiko alikuwa busy sana kutafuta pesa yakutulisha nyumbani na kunisomesha pia ikiwa ndugu zangu walikuwa hawana kazi yeyote na wala sikujali kabisa maumivu ya mama yangu wala ndugu zangu kuna siku mama yangu aliniambia kuwa nimebadilika sana na kama na mwanaume basi najidanganya kwani mimi bado mdogo na hakuna atakaye nipenda na kunioa wakati ata kidato cha nne sijamliza japo baadhi yao huwa wanaolewa na aliniambia kitu ambacho kiliniumiza sana baba yako amefariki tokea kidato cha kwanza na kusomesha mimi na hujali kabisa unafeli hakuna ata ndugu yako aliyowayi kuleta peni yako ya shule wewe endelea siku nikifa utaijua dunia ilivyo na huyo anayekudanganya ndoutamjua vizuri..nilimwambia mama samahani kama nimekosea lakini mimi sina mwanaume na nikamuahidi kufaulu vizuri kidato cha nne.Kwakweli siku ambayo sitosahau ni huyu kaka kuniita kwake na kunibaka na ikiwa nilibakiza siku mbili ili niingie kwenye chumba cha mtihani aliniambia kuwa hawezi kuvumilia nikimaliza shule nitakuwa busy sana nanitakuwa simjali tena niliumia kiukweli lakini sikuwa na jinsi muda ulipopita alipa sh.2000 nakuniambia niende nyumbani yeye kapata dharula katika kazi zake kiukweli nilishangaa kauli hiyo lakini nikahisi ni kweli na nikanyanyuka kwa maumivu na kuamua kuoga kabla ya kwenda nyumbani ili mama asijue chochote,nilipo maliza kuoga niliondoka na nilipofika nyumbani nilienda moja kwa moja chumbani kwangu na kulala ili mtu yeyote asinisumbue niliamka usiku wakati wa kula lakini kwa kuzuga nilisema naumwaa sana siwezi kwenda sebleni nahisi kizunguzungu nikaomba nilie chumani na ujanja wangu ulifanikiwa nikala na kulala.Nilifanya mtihani wangu japo nilijua sitofaulu kwa mawazo niliyokuwa nayo juu ya jambo hilo na pia yeye alibadilika kuazia siku ile aliyonifanyia tendo la uovu bila mimi kupenda,nilimaliza mitihani yangu na kuendelea na mambo yangu lakini baada ya miezi kadhaa kupita niligundua kuwa na ujauzito na siku hiyo niliyojua mjamzito mama yangu alinikuta na simu nakuniuliza baadhi ya maswali na kukua message ambazo nilikuwa namtumia mpenzi wangu kuwa najihisi vibaya na sijui nini cha kufanya labda naweza kuwa na mimba yake ,mama aliaza kulia kama amefiwa mpaka kina dada walipokuja nakuaza kunichangia kwa maneno makali na kusababisha kwenda kununua kidude cha kupimia mimba na kweli nilikutwa na ujauzito mama yangu kipenzi Beatrice alidondoka hapo hapo kwa mshituko na kuaga dunia(kufariki) kitu ambacho ndugu zangu walinikataa kabisa na nikakimbilia kanisani nakupata msamalia ambaye alinipa kibarua cha kufanya kwake na mchungaji nakumbuka alienda nyumbani kwetu kwa miaka kadhaa kupita ambayo nilikuwa sihishi nyumbani ili kuniombea radhi kwa ndugu zangu nilipata nafasi ya kuingia chuo kwa sasa nashukuru kwani na maisha manzuri ikiwa na ndugu zangu nao wana biashara zao ata mwanangu anasoma shule na Yule mwanaume nilisikia kuwa amefariki na ukimwi,lakini kamwe siwezi kusahau picha ya mama yangu na ninajutia sana kwa kutomsikilza kwa maneno yake aliyoniambia.


                                     mwishoooooooo
Post a Comment
Powered by Blogger.