HAKIKA SITOKUSAHAU!!!

MTUNZI: Dorcas Safiel.
 SEHEMU YA TATU;
HAKIKA SITOKUSAHAU!!


 TULIPOISHIA
Nancy ametoka kuamka na  kuwaangalia ndugu zake na kukuta hawapo na alipoenda nje akamkuta mlinzi na akamuulizia akamjibu kuwa wametoka lakini hawajui wameenda wapi,anahamua kurudi ndani kuchemsha chai na kusubiri warudi.

TUENDELEE
 Muda mchache baadaye nilikuwa bado natafakari kuhusu ndugu zangu kwani si kawaida yao kuondoka asubuhi muda kidogo nilisikia mlio wa gari ukiwa unaingia ndani na sikutaka kusubiri na nikahamua kutoka ili niende kuwaona ndugu zangu na kuwauliza walipotoka,nilienda nje na nikamkuta mary pamoja na lilian wakiwa wako kwenye hali isiyokuwa nzuri nilipatwa na mshituko kidogo na kuwauliza 'shikamooni,mbona mko hivyo kuna usalama kweli?' 
 hawakunijibu ata mmoja wao na kuhamua kuingia ndani bado nilikuwa kwenye bumbuwazi kwani sikujua nini kipo nyuma ya pazia tulipofika sebleni mary aliaza kuongea "nancy usiku wa jana mama alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemjua na alimwambia kuwa....!!" dada alimeza mate kidogo nakuaza kulia kwa uchungu bila kuvumilia tena yale ya moyoni " NANCY BABA HAYUKO TENA DUNIANI' nilihisi kama niko kwenye ndoto na ninahitaji kuamka lakini nashindwa kwani ni ukweli niliaza kulia kwa nguvu na kumuuliza " baba kweli amekufa ?acha utani dada baba hawezi kufa" kiukweli hakuna ambaye alikuwa yuko kwenye hali nzuri na ukiangalia ata mazingira ya nyumba yetu yalikuwa yamejitenga sana mlinzi ndo alikuwa amekuja ndani pamoja na dereva kututuliza ili tusijaze watu, baada ya dakika chache nilisahau ata kama na mama dunia hii lakini ghafla nikamkumbuka mama nakuuliza kuhusu hali yake na wamempeleka wapi niliambiwa kuwa mama yuko hospitali kalazwa na hali yake si nzuri..mlinzi alisema tunabidi tupigie ndugu ili waweze kuja pale nyumbani aliweza kuchukua simu ya dada lilian ambaye ndo dada yangu wa kwanza na akawapigia baadhi ya ndugu baada ya nusu saa ndugu baadhi walikuwa wamefika majonzi yakatawala katika nyumba yetu kila mtu na kilio chake nakumbuka baada ya siku moja kutoka kupata taarifa hiyo tulibebwa mpaka hospital ambayo mama alikuwa amelazwa nilipofika na kumuona mama yangu alikuwa kama kichaa kwani alikuwa anaongea maneno yasiyoeleweka kabisa na kutaja jina moja tu la baba yangu nilishindwa kuvumilia na kuamua kutoka nje na muda kidogo kina dada na kina shangazi pamoja na mamdogo waliturudisha nyumbani.

 Ndugu wengine wakiume waliaza kupanga taratibu za mazishi na mwili wa baba yangu kurudishwa nyumbani dar-es-salaam. Baada ya uchunguzi baba yangu ilionekana alivamiwa na majambazi ambao walimwinda siku ambayo alikuwa anatokea bank kuchukua pesa ambapo alikuwa anajiandaa na safari ya kurudi nyumbani,
Baada ya siku 3 mwili wa baba ulikuwa tayari umefikishwa na mama kidogo sana alikuwa na nafuu katika kumzika mume wake kipenzi sana. Tulimzika baba yetu na maisha yakaendelea japo sio kama yale ya zamani ya furaha sana na kumwamini Mungu kwa kila jambo ambalo lilikuwa mbele yetu, kabla ya 40 ya baba ndugu walihitaji vitu vyote vinavyomuhusu baba yangu na kutuhamuru kuwapa kila kitu kasoro hati ya nyumba tu tunayoishi sisi kwa kutuhurumia tu..
Mama hakuwa na jinsi aliwapa kila walichoitaji na maisha yakaaza kushuka, nilipoanza sekondari nakumbuka maisha niliyozoeshwa nyumbani na wazazi wangu kipindi nikiwa shule ya msingi na sasa ni tofauti   sana na nikaaza kujiunga na makundi mabaya ili tu kukidhi mahitaji yangu binafsi kama nancy..

MIEZI KADHAA NANCY UNAJUA ALIKUAJE!!! ENEDELEA KUFUATILIA HADITHI YA HAKIKA SITOKUSAHAU.;
 
Post a Comment
Powered by Blogger.