HADITHI | HAKIKA SITOKUSAHAU!!!! MTUNZI; DORCAS SAFIEL.

SEHEMU YA KWANZA....


 Haya ndo maisha yangu japo sikutaka wengi wayajue lakini sina jinsi kwani nataka dunia ijifunze kupitia mimi,natumai utakapomaliza kusoma utakuwa umeelewa kidogo japo si sana share kwa jinsi unavyoweza ili kila mtu aweze kufundishika..
Mimi ni mtoto wa pili katika familia ya Daudi jina langu ni Nancy shule ya msingi niliosoma katika shule ya Hekima na kumaliza darasa la saba kwa miezi hiyo kadhaa ya kusubiri matokeo yangu ya mtihani nilioufanya mwenzi wa 9, nilikuwa tu nyumbani bila kufanya kitu nami ukizingatia nimebahatika kuwa na dada wawili walionitangulia duniani nami nikiwa kama mtoto wa mwisho na familia yetu ilikuwa ya kitajiri katika sehemu moja iliyoitwa Masaki mkoani Dar es salaam nakumbuka siku moja nilipokuwa nimeamka asubuhi ili ninywe chai kichwa kilikuwa kinauma sana nikajua ni kitu cha kawaida na kwenda sebleni ambapo si mbali na chumbani kwangu nilikuta dada ndo anahitaji kusali ili aaze kunywa chai nakama kawaida ya nyumbani kwetu huwezi kula bila kusali na kumaliza kula unabidi ushukuru yani familia yetu ni familia ya kidini zaidi nilimsogelea na kumuamkia "shikamoo dada mary,umeamkaje asubuhi hii natumaini mungu bado ni mwema kwako"?.
 dada alinijibu kwa tabasamu "marahaba Mungu mwema kwetu wote karibu tunywe chai". tuliaza kwa maombi na kuendelea kunywa chai ambapo meza ilikuwa imetawala vitu mbali mbali kama mikate ya kuoka,chapati pamoja vitumbua ili kila atakaye penda kula basi aweze kula pamoja na juice ya embe ambayo nyumbani tulipendelea sana kunywa juice asubuhi kuliko kunywa chai.. tulipomaliza kunywa chai nilimuambia dada kichwa kinauma sana akaniambia kuwa niombe tu mungu atatenda kwa wakati.
nilimuuliza dada lilian kaenda wapi mbona asubuhi sana na sijamuona au yuko chumbani kwake?,hapana kaenda shopping na mama kununua vitu vya ndani alafu atarudi navyo yeye.baada ya mazungumzo hayo nilinyanyuka na kwenda chumbani kwangu kupumzika kwani kazi ndogo zote zilikuwa zimeshafanywa maisha yaliendelea na siku kuyoyoma mpaka mwenzi wa 12 ya mimi kupata matokeo yangu ili kujua niko upande gani kama kusuka au kunyoa na kwa kipindi hiko baba yangu alikuwa amesafiri kikazi Nairobi na kwa hamu kubwa alihitaji kujua kama mziwanda wake nimeweza kufaulu!
wiki mbili kabla ya matokeo ya darasa la saba nilifanyiwa birthday nyumbani na ilikuwa nzuri kwani watu wengi walikuja na ndugu zangu pia,sherehe ili pendeza sana na nilikuwa na zawadi nyingi pamoja na husia wa mama yangu aliosema " mwanangu nancy mtoto niliyekuzaa kwa kisu yaani upasuaji nakupenda sana na wewe kuonyesha kwako kunipenda kutaambatana na kujitunza kwako pia na kuniheshimu kwa mambo yote nitakayokuambia na mwisho kumbuka wewe ni mnzuri na ni kipenzi changu pamoja na ndugu zako." nilisema neno moja kwa mama " nakupenda sana mama".usiku ulizidi na sherehe ikaisha watu baadhi walibaki nyumbani kwa kuogopa wezi njiani.
baada ya wiki mbili kufika matokeo yangu yalitoka na kuambiwa nabidi nikaangalie kwani sikutaka mtu yeyote ajue namba yangu ya mtihani zaidi ya baraza la mitihani.. sikuweza kwenda kwa siku hiyo nikaenda siku nyingine nilipofika kila mtu nilimkuta na hali yake mwingine alilia, kucheka,tabasamu na ata shangwe nilimuona rafiki yangu anayeitwa racheal nilimsalimia nakumuuliza vipi rafiki matokeo? alinitazama kwa huzuni na kuniambia "nimefeli rafiki yangu" aliangua kilio nikabidi kuona huruma na kumsogeza pembeni kumtia moyo kabla yangu sijayaona alipopata nafuu alisema" asante wewe yako vipi umeyaona lakini"?
 nilimwambia sijaona ndo kwanza naenda kuyaangalia nilimuaga na kuondoka zangu nilipo fika kwenye ubao wa matangazo na kuaza kutafuta jina langu kama robo saa ni kaona uwiiiii moyo ukalia PAAAAAAH!!!

UNAJUA NINI KILITOKEA KWA NANCY MATOKEO YAKE YALIKUAJE UNGANA NAMI JUMATATU KUKUJUZA ZAIDI!.
Post a Comment
Powered by Blogger.