ASKARI POLISI WA FFU IRINGA KUHUKUMIWA KIFO.
MAHAKAMA Kuu kanda ya Iringa inaendelea na vikao vya kusikiliza kesi ya mauaji ya mwanahabari mkoani Iringa Daud Mwangosi inayomkabilia mtuhumiwa wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Pasificus Cleophace Simon mwenye namba G 2573.
296587_4672851945587_1395901855_nAskari wa kikosi cha kutuliza ghasia walipokuwa wamemshikilia Daudi Mwangosi
Aidha mahakama hiyo imetaja siku ya tarehe 21 mwezi wa 7 mwaka huu kuwa ndio siku ya kutoa hukumu ya kesi hiyo inayomkabili askari wa jeshi la polisi kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) Pasificus Cleophace Simon.
Taarifa zinaeleza kuwa endapo mtuhumiwa wa mauaji ya Daudi Mwangosi atapatikana na hatia ya kutenda kosa hilo basi atahukumiwa kunyongwa hadi kufa.
582728_4673002029339_659749645_nMwandishi wa habari, Daudi Mwangosi akiwa kazini enzi za uhai wake.
Inadaiwa kuwa Daudi Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Post a Comment
Powered by Blogger.