FAIDA ZA MAZOEZI MWILINI.

  •   ni kuongeza nafasi ya kuboresha umri wa kuishi na kuishi katika afya njema.
  •   mazoezi yanasaidia kutulinda na magonjwa ya moyo, kiharusi na magonjwa yanayoambatana nayo kama shinikizo la damu na ongezeko au kiwango cha juu cha lehemu katika damu. Kiwango cha juu cha lehemu katika damu kimekuwa kisababishi cha ongezeko la shinikizo la damu na hata kuwa katika hatari ya kupata kiharusi.
  •   mazoezi yanatusaidia kuepukana na magonjwa ya kansa fulani kama kansa ya tumbo, kansa ya matiti, kansa ya mapafu na kansa ya kizazi. Hii ni kwa sababu mazoezi yanaboresha mifumo mbali mbali ya mwili na kuwezesha mwili kutoa taka na sumu mbali mbali mwilini, pamoja na kuimarika kwa kinga ya asili ya mwili.
  • Tafiti za wanasayansi zilizofanyika hivi karibuni zinaonyesha kuwa mazoezi yanasaidia kutokupoteza uwezo wa kuona. Matatizo mengi ya kuona hujitokeza mara nyingi kwa wazee, kwa hiyo tunaweza kuzuia hali hiyo isijitokeze kwa kufanya mazoezi.(kwa mujibu wa jarida la newscientist la marekani)
  • mazoezi yanasaidia kutukinga na kisukari aina ya pili (ugonjwa ambao mtu anaupata ameshakuwa mkubwa na sio kwa kuzaliwa), na kutukinga na matatizo ya mmeng’enyo ambayo yanaweza kutuletea magonjwa ya moyo na kisukari pia.
  • Mazoezi yanasaidia pia kutukinga na matatizo ya mmomonyoko wa mifupa (osteoporosis) ambayo mara nyingi hujitokeza uzeeni. Yanaimarisha afya ya akili, yanasaidia kutuepusha na magonjwa ya kupoteza kumbukumbu hasa kwa wazee. Pia mazoezi yanatuondolea msongo wa mawazo, woga na mtu kuwa katika afya nzuri ya akili.
  • Mazoezi yanasaidia kuwa na mapafu yenye kufanya kazi vizuri,moyo wenye afya na kuimarisha misuli ya mwili kwa ujumla. Bila kusahau kuwa mazoezi husaidia kupata usingizi mzuri kwa afya bora.
Post a Comment
Powered by Blogger.