UFAHAMU UVIMBE KATIKA KIZAZI CHA MWANAMKE.


FAHAMU UVIMBE KATIKA KIZAZI CHA MWANAMKE(UTERINE FIBROIDS|LEIO MYOMAS)

 Fibroids ni nini?
 Ni aina ya vivimbe vinavyoota kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi,Tatizo hili huwakumba wanawake wengi ambapo huwapata kwa 5% wanawake wenye umri wa miaka 20-30 hadi 30-40 na zaidi ya 40% ni kwa wale wenye umri zaidi ya 40 hivyo kwa ujumla tatizo la fibroids huwapata wanawake wengi hasa katika umri wa kuzaa(reproductive age) hii ina maana kuwa kadri umri unavyokuwa mkubwa mwanamke ana nafasi kubwa kupata uvimbe huu.
Tafiti zinaonyesha kuwa tatizo hili huwapata zaidi wanawake wa kiafrika kuliko wazungu pia huwapata zaidi wanawake ambao hawajazaa kabisa au wale ambao wamekaa muda mrefu bila kuzaa,pia wanawake wanene,na wale waliopata hedhi mapema wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu.

                                   AINA KUU ZA FIBROIDS
Uvimbe huwa na ukubwa tofauti kwani huanza mdogo na baadaye huwa mkubwa sana na hata wakati mwingine huonekana kwa mwanamke mjamzito kwani uvimbe huu huweza kuwa mmoja mkubwa  na wakati mwingine huwa zaidi ya mmoja na kutanda katika mfumo wa kizazi.

                                  CHANZO CHA TATIZO.

Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi ila kuna sababu ambazo huweza kusababisha mwanamke kupata fibroids,sababu ambayo ni common kusababisha tatizo hili ni wingi wa homoni ya OESTROGEN ambao ipo katika mwili wa mwanamke na ndiyo hufanya kazi ya kusababisha mwanamke kupata hedhi pia mara nyingi uvimbe huu hukua mkubwa sana kipindi cha ujauzito kwasababu vichocheo vya OESTROGEN huongezeka na kuwa vingi ili kulinda makuzi ya mtoto pia ni mara chache watu walio kikomo cha hedhi kupata fibroids na wakipata kuna hatari ya kuwa na kansa.                          DALILI ZA FIBROIDS 

Dalili za uvimbe katika kizazi cha mwanamke hushindwa kuonekana iwapo uvimbe ni mdogo na pia dalili hutegemea sehemu ilipo kwenye mfuko wa kizazi pia na ukubwa wake,pamoja na hayo dalili zake ni kama zifuatazo;

1.kutokwa na damu yenye mabonge kwa muda mrefu

2.kutokwa damu katikati ya mwenzi na hedhi kutokuwa na mpangilio.

3.kupata maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi.

4.kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

5.kupata maumivu makali ya mgongo.

6.hukojoa mara kwa mara.

7.mimba kuharibika mara kwa mara.

8.kupungukiwa na damu mara nyingi.

9.miguu kuvimba. 

10.mkojo kubaki kwenye kibofu.

11. haja kubwa kuwa ngumu .

                 MATIBABU\VIPIMO

 Matibabu ya fibroids hufanyika kwa daktari kumkagua mgonjwa kwa kutumia mikono miwili au kupima pia anaweza kutumia kipimo cha ULTRA SOUND ya nyonga kwani ni rahisi kugundua uvimbe au kipimo MRI,
matibabu huweza kulenga ya kutibu dalili au kupunguza uvimbe na pia iwapo mwanamke ana tatizo hili na hamna dalili zozote basi kutumia dawa kwasababu mwanamke anapofika kukosa hedhi tatizo hili hutokea.
Wanawake wengi wana fibroids ndogo ndogo ambazo hazina dalili hivyo hushindwa kutambua mpaka pale wanapo beba ujauzito au kupima ndio hugundulika.

                NJIA ZA KUTIBU UVIMBE MKUBWA 
1. DAWA- hapo mgonjwa hupewa matibabu ya dawa ambazo hurekebisha kiwango cha homoni ya OESTROGEN mfano wa dawa hizo ni DANAZOL na aina ya pili ni vidonge vya kutuliza maumivu ya fibroids.

2.UPASUAJI-upasuaji hufanyika kwa kutegemea na ukubwa wa uvimbe na wingi wa fibroids ambapo upasuaji huo ni wa aina mbili.
A.MYCOMECTOMY- hii ni njia ya upasuaji hutumika kwa mgonjwa mwenye uvimbe mmoja mkubwa ulio katika sehemu nzuri na upasuaji hutumika kwa mgonjwa mwenye uvimbe mmoja mkubwa ulio katika sehemu nzuri na upasuaji wa njia hii uvimbe una nafasi kubwa kurudi.
B.TOTAL ABDOMINAL HYSTERECTOMY-hii ni njia ya upasuaji ambapo kizazi kina uvimbe mmoja mkubwa sana au vivimbe vikiwa vingi vingi.
                  
                  MADHARA YA FIBROIDS
a. Husababisha mimba kutoka mara kwa mara na hatimaye mtu kuwa mgumba.

b. Husababisha saratani ya shingo ya kizazi.

NOTE; Una shauriwa kwenda kupima afya yako ili kujua kuwa una tatizo gani katika mwili wako kabla tatizo halijakuwa kubwa katika mwili wako na kukuletea madhara mengine katika mwili wako.
  
Kwa ushauri na matibabu zaidi piga namba 0717-035770 au 0753692612.    
Post a Comment
Powered by Blogger.