Dodoma Ugonjwa Wa Ajabu Waibuka 7 Wamefariki Na 21 Wamelazwa.


Waziri wa afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto mhe Ummy Mwalimu

Na Dorcas Safiel
Ugonjwa wa ajabu umeibuka katika wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma na kuua watu saba na wengine 21 wamelazwa.Ugonjwa huo dalili zake zikiwa ni kutapika, kuharisha, kupata rangi ya manjano machoni na sehemu zingine na tumbo kuvimba na kujaa maji.Akizungumzia kuibuka kwa ugonjwa huo ambao umezua taharuki kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto mhe Ummy Mwalimu amesema tayari sampuli zaugonjwa huo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya uchunguzi huku akiwatoa hofu wakazi wa mkoa huo ambao wanahisi huenda ukawa ni ugonjwa wa kimeta.Mbali na kushambulia binadamu lakini pia ugonjwa huo umezuru wanyama wafugwao wakiwemo mbwa na paka.Kwa upande wake Dk. James Chalz Mganga Mkuu wa mkoa wa Dodomaanasema bado wataalam wa magonjwa mkoani Dodoma wanaendelea na uchunguzi huku akidai kuwa wagonjwa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamojana hospitali ya wilaya ya Kondoa.
Post a Comment
Powered by Blogger.