Brazil Yafufuka Yapiga Mtu 7 COPA AMERICA,Phillipe Coutinho Moto Na Peru Na Ecuador Ngoma Mbichi.

Michuano ya Copa America imeendelea tena usiku wa leo kwa mechi mbili kuchezwa zikiwa za kundi D nchini Marekani.
Mahabiki wa Brazil.
Brazil kama wamelipa kisasi cha mabao 7-1 toka kwa Ujerumani 2014 kwenye kombe la Dunia walivyofungwa huku wakiwa wenyeji kwa kuifunga timu ya Haiti mabao 7-1 kiungo mshambuliaji wa Liverpool Phillipe Coutinho alikuwa mwiba kwa Haiti baada ya kupiga Hat Trick katika michuano hiyo katika dakika ya 14,29.na 90.
Phillippe Coutinho.
Naye mshambuliaji anayekuja kwa kasi Renato Augusto kidogo naye aondoke na mpira baada ya kufunga mabao mawili mnamo dakika ya 35 na 86.
Renato Augusto.
Mabao mengine ya Brazil yamefungwa dakika ya 59 Gabriel na dakika ya 67 Lucas Lima na bao la kufutia machozi la Haiti limefungwa na James Marcelin mnamo dakika ya 70 hadi dakika 90 zinamalizika Brazil 7 Hait 1.
Gabriel.
Lucas Lima.
Mchezo mwingine wa kundi hilo umechezwa Alfajili ya Leo ambapo umezikutananisha Ecuador na Peru na mchezo huu kumalizika kwa sare ya kufungana 2-2.
Peru walikuwa wa kwanza kupachika bao mnamo dakika ya 5 kupitia kwa Christian Cueva na katika dakika ya 13 Peru walipata bao la pili likifungwa na Edison Flores na dakika ya 39 Winga hatari wa West Ham Enner Valencia aliiandikia bao timu yake ya Ecuador hadi mapumziko Peru walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Christian Cueva.
Edison Flores akipongezwa.
Enner Valencia.
Kipindi cha pili kilianza kwa Ecuador kutaka kusawazisha huku Peru wakitafuta bao la tatu mnamo dakika ya 49 Miller Balanos aliisawazishia Ecuador hadi 90 timu hizi zimetoka sare ya 2-2 na kulifanya kundi hili timu ya Brazil ikiongoza ikiwa na pointi 4 sawa na peru yenye pointi 4 zikiwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Miller Balanos.

Post a Comment
Powered by Blogger.