HAKIKA SITOKUSAHAU!!

MTUNZI; Dorcas Safiel.
 SEHEMU YA PILI...
 HAKIKA SITOKUSAHAU.

TULIPOISHIA...
Nancy alipoenda kwenye ubao wa matangazo na alichokiona moyo wake ukalia paah yaani hakuamini na kile kilichokuwa mbele ya macho yake.

MWENDELEZO'

Nancy hakuamini kabisa kuwa amefaulu kwenda sekondari kwani alijua angeweza kufeli kama rafiki yake hakutaka kuendelea kukaa pale na moja kwa moja kwenda kwenye gari ambalo aliletwa na dereva wa nyumbani!
  ahaa kaka Mungu ni mwema nimeweza kufaulu vizuri sijui baba atanipa nini kwa kweli maana mmmh! ni ajabu sana kwangu rafiki yangu yule kipenzi kafeli... nancy alimaliza kuongea huku akishusha pumzi kwa maelezo aliyoyatoa 
hongera mdogo wa mie kazana zaidi kwani unafikiri baba atakupa nini ?  nancy alijibu sijui lakini huku wakiwa njiani wanaendelea na safari ya kurudi nyumbani baada ya dakika chache walikuwa washawsili nyumbani hakutaka ata kwenda chumbani kwake moja kwa moja alienda kwa dada zake aliowakuta sebleni wakiwa wanaangalia movie ya (the sky ) aliaza kuita dada dada dada jamani siamini nimefaulu mwenzenu alafu rafiki yangu amefeli ndo cha ajabu 
liliani alijibu   hongera,  mama na baba watafurahi sana kwa kweli kwani ndo tegemeo uliyebaki kwenye familia yetu endelea hivyo hivyo usije kututia aibu umesikia? ndiyo dada asante nimesikia na nitatendea kazi kwa kweli 
mary naye hakuwa nyuma kumtakia mdogo wao mpendwa hongera aliyostahiri kwani kuna walio wengi walikuwa wamefeli kwa mwaka huu na toleo la pili kutokuwepo kabisa tofauti ya miaka mingine nyuma..
USIKU..
 mama yao aliporudi nyumbani aliwakuta watoto wake wakiwa kwenye makochi wamestarehe kila mtu akiwa na shughuli yake mwingine akiwa na remote akibadili channel mwingine akiperuzi kwenye mitandao lakini nancy akiwa ameshika novel yake akiisoma alipomuuona mama yake tu alirusha kitabu na kwenda kumuwaoo na kuanza kuongea bila kuweza kuvumilia kuchoka kwa mama yake " mama nimefurahi sana najua ushajua nimefurahi kwanini kwasababu wewe mama yangu  "
" Nancy jamani ata sijapumzika looh aya najua kwasababu umefaulu au mama kakosea"
 hahaha mama umepatia naomba zawadi yangu na nimpigie baba simu ili kumwambia aniletee zawadi akitoka safari.
  mama yake bila hiana alimpa simu na kumpigia baba yake na kumtaarifu juu ya matokeo kiukweli mzee Daudi alifurahi sana na kumuahidi kumpatia zawadi atakaporejea katika safari yake ambayo alikuwa anahitmisha baada ya wiki moja !!
usiku ulipozidi kukimbia ili siku nyingine iweze kuja na miezi kuweza kukimbia waliamua kula, kusali na kwenda kulala huku kila mmoja akiwa na chumba chake..
ASUBUHI..
9;00 nancy akiwa anaamka chumbani ili kwenda kunywa chai kama kawaida yake akakuta amna mtu ndani aliita bila mafanikio kuitkiwa alienda jikoni lakini pia hakumkuta mtu akenda mpaka nje kwa mlinzi na kumkuta na akaamua kumuuliza ndugu zangu wameenda wapi? mlinzi alijibu" wameondoka lakini sijui wameelekea wapi" kwa kweli ikiwa bado ana msongo wa mawazo wakutojua ndugu zake wameelekea wapi alirudi ndani na kuamua kwenda uchemsha chai ili aweze kunywa na kusubiri tukio hilo kwake lilikuwa la ajabu kwani hakuwayi kutokea ndugu zake kuondoka wote asubuhi..

TUKUTANE KESHO ILI TUJUE WALIENDA WAPI ASUBUHI ASUBUHI.....
Post a Comment
Powered by Blogger.