SOMA CHANZO CHA MTOTO DUNIANI.
Na Dorcas Safiel; 

Kila mwanamke hutamani siku moja kuwa na mtoto wake akiwa wa kike au wakiume karibu kwenye website hii ya seetheafrica ili nikujuze chanzo cha ujauzito, dalili na hatua ya mwisho kabisa kwa kumzaa mtoto ambaye dunia hufurahi kumkaribisha kiumbe huyo.
   
   CHANZO CHA UJAUZITO.
Mwanaume huweza kumpatia mwanamke pale tu atakapo balehe kuanzia miaka 14 na kuendelea lakini pia mwanamke huweza kupata mimba akiwa katika siku zake hatari za hedhi baada ya kupata mzunguko wake siku za hedhi.Mwanamke katika majira ya hedhi mwili wake huangua yai kila mwenzi,kutoka sehemu ya kiungo cha uzazi kinachoitwa ovari na kusafiri taratibu kupitia mirija ya uterasi kwa muda wa siku 8 hadi 12 kuelekea nyumba ya uzazi,Mwanaume anapofanya tendo la ndoa mbegu zake hubeba mamilioni ya mbegu na moja tu inapokutana na yai ndipo mimba hutungwa..
Katika utungaji mimba huweza kupata mtoto wa kike,kiume mapacha wa kufanana au wasiofanana hiyo ikwa inategemeana na chakula ambacho unakula kabla ya siku chache ya kukutana na mwenza wako au kwa kufuata njia za daktari wa uzazi.

DALILI ZA UJAUZITO.

  Ni mabadiliko katika siku zako ambazo huwezi kuona hedhi kwa mwenzi ambao unafuata-pia unaweza kushika mimba ukaendelea kuona damu mwezi huo, Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza kwenye kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa kwenye ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo amabazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango na siku za damu hubadilika.

Ni kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa. Hii inasababishwa na ongezeko la homoni za istrogen pale unapokuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza. 

 Ni kichefuchefu na kutapika. Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapoToka kulala. Hii ni kwa sababu ya homoni ya ‘projestroni’ ambayo husababisha kupungua nguvu kwa misuli ya mrija wa chakula au koromeo.

Uchovu usiokuwa na usingizi usiokuwa na sababu. Hii hutokea kwa sababu ya ongezeko la homoni ya ‘projestroni’ na mama utajikuta unasinzia mara kwa mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba ila hata kipindi cha mwisho wa mimba hujisikia uchovu.

Kusumbuliwa na harufu mbalimbali. Hasa kama unapata mimba kwa mara ya kwanza, utachukia harufu za vyukula na vinywaji mabalimbali. Wakati mwingine hata harufu za watu walio karibu nawe zinaweza kukukera. 

 Ni kujaa gesi tumboni. Utaona baadhi ya nguo zako zinakubana zaidi hasa sehemu ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi mwilini zinazokufanya kijisikia tumbo kujaa.

Kukojoa mara kwa mara. Hii kwanza hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini ambayo huongezwa na homoni za ujauzito makusudi kutoa rishe ya kutosha kwako na kwa kiumbe tumboni. Ukiwa na damu nyingi pia utakojoa sana za kikemia mwilini. Pili utajisikia kwenda haja ndogo mara nyingi pale kiumbe kitakapoongezeka na kubana kibofu cha mkojo.

Kuongezeka kwa joto la mwili. Kwa kina mama ambao hupima joto lao kama njia ya uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na nusu mfurulizo.

 Kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha karatasi ngumu. Famasi nyingi huuza vipimo ambavyo ikikichovya kwenye mjojo wako huweza kugundua homoni za mimba kwenye mkojo,
hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani hata kazini. Kipimo hiki ukisha kichovya kwenye mkoja kama katatsi inavyoelekea utaona mistali baada ya dakika moja inajitokeza upande wa chini,
Ikitokea mistari miwili basi unaweza kuwa na mimbaKulingana na kiwango cha homoni mwilini, kuna kina mama hakionyeshi majibu mpaka upitishe wiki moja bila kuona siku zako.

NB;Pamoja na dalili hapo juu, unatakiwa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.


 HATUA YA MWISHO
Mtoto anapokuwa tayari kuzaliwa misuli ya mfuko wa uzazi huaza kujikunja na kujikunjua hali ambayo huifanya misuli ya uke wa uzazi pia kutanuka ndipo uchungu huazia hapo,inapofika wakati fulani kondo ya uzazi( chupa) ambayo inamuhifadhi mtoto hupasuka na maji( ute) kutoka ukeni kwa nguvu na ndiyo njia ambayo mtoto hupitia wakati wa kujifungua.
Jinsi kasi ya misuli inavyojikunja na kukunjuka na ndivyo maumivu huzidi na kufanya shingo ya mfuko wa uzazi kufunguka,wakati ikifunguka na kufikia cm10 mwanamke hupatwa na hisia za kusukuma mtoto,kwa kawaida mtoto huaza kutoka kichwa na kumalizia miguu akiambatana na kilio kinachomfanya kupanua njia za kuvutia pumzi,kitovu kilichomuhunganisha yeye na mama yake hukatwa na ndiyo chanzo kikubwa kwa mtoto cha kumfanya kula angali alipokuwa tumboni na maisha yake huanzia hapo........
    

Post a Comment
Powered by Blogger.