Bingwa Wa Dunia Usain Bolt Kupokonywa Medali Yake Kisa Hiki Hapa.

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 100 na 200 Usain Bolt huenda akapokonywa mojawapo ya medali yake ya dhahabu alioshinda katika michezo ya Olimpiki mjini Beijing 2008.

Imeripotiwa na chombo cha habari cha reuters kwamba violezi vya mmoja wa washiriki katika kikosi cha Jamaica kilichokimbia mbio za kupokezana vijiti za 4 mara 100 ,Nesta Carter alipatikana na dawa ya kusisimua misuli.

Habari hizo zinajiri baada ya kupimwa tena kwa violezi 454 kutoka kwa michezo hiyo ya 2008.
Carter ambaye pamoja na ajenti wake hawakutoa tamko lolote atawekewa vikwazo iwapo violezi vya pili vitapatikana na dawa hizo.
Post a Comment
Powered by Blogger.