BASI LA NBS LAPATA AJALI NA KUUA MKOANI MOROGORO.

Na Dorcas Safiel
 Huko mkoani Morogoro ajali ya basi la kampuni la Nbs lililo kuwa likitokea mkoani Dar es salaam kuelekea tabora limeacha masikitiko na kilio kwa wengi  baada ya kuacha njia na kupinduka katika eneo la Tab hotel tarafa ya Gairo wilayani Gairo mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu watano wakiwemo watoto wawili na wengine ishirini na sita majeruhi.
 Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya  ya Gairo Dk.Mushi Mabura ameeleza namna alivyopokea majeruhi hao kumi na tatu wa kike akiwemo mama mjamzito  na mtoto mmoja na kumi na tatu wakiume akiwemo mtoto mmoja pia alisema kuwa waliofariki wamewapokea watano wakiwemo wanaume wawili na wanawake watatu na waliozidiwa kwa ajili ya kupelekwa hospitali ya rufaa Morogoro ni watu saba wakiwemo  wanaume watano na wanawake wawili, nalo jeshi la polisi mkoani morogoro limezibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo miili ya marehemu imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya rufaa mkoa wa morogoro..
Post a Comment
Powered by Blogger.