BABA ACHORA TATOO ILIYOFANANA NA UPASUAJI ALIOFANYIWA MTOTO WAKE
Baada ya mtoto wake kufanyiwa upasuaji kichwani ili atibiwe saratani (cancer) alibakiwa na kovu kichwani kwake upande wa kulia, na stori hii imetrend sana kwenye mitandao ya kijamii duniani.

Gabriel Marshall(8) aligundulika kuwa na saratani ya ubongo inayofahamika kitaalam kama anaplastic astrocytoma ilikuwa mwezi Machi 2015. Upasuaji wa kuondoa saratani hiyo ulifanyika lakini amebakiwa na kovu kichwani kwake, ameeleza baba yake anayeitwa Josh Marshall.
 
“Mtoto wangu alikuwa akiwaza sana baada ya kufanyiwa upasuaji, alijihisi sijui ni kama mnyama gani mbaya akiona lile kovu” Baba mtoto Marshall aliiambia ABC News.

Mwezi Agosti 2015, Marshall aliamua kuchora tattoo ambayo itafanana na kovu la mtoto wake . “Nilisema, Unajua nini, nitachora tattoo aina ya kovu la mtoto wangu kichwani, kwa hiyo mtu akimuangalia lazima ataniangalia na mimi” Alisema. Gabriel anaipenda tattoo alichora baba yake na anawaambia watu yeye na baba yake ni kama mapacha.

Uamuzi wa Marshall haujamfanya tu mtoto wake kujiamini, lakini pia anapokea sifa nyingi baada ya kuweka kwenye mashindano ya St. Baldrick Foundation #BestBaldDad, ambapo kuna wababa 55 ambao wamenyoa vipara wakuwasupport watoto wao ambao wana saratani, picha ya Marshall ilikuwa na maneno yaliyoandikwa “Mimi na mtoto wangu katika shindano la mwaka huu la St. Baldrick hapa Wichita, Kansas, Nimechora tattoo ya kovu la mtoto wangu kumfanya asione ni kitu kibaya”.

Marshall na mtoto wake walipata kura zaidi ya 5,000 na kushika nafasi ya kwanza.
“Sikukusudia ili iwe kitendo kikubwa kiasi hiki, ilikuwa ni shindano la urafiki kati ya watu  ambao wanaugua saratani katika kutoa support kwao”

Gabriel anaendelea vizuri, Marshall aliiambia ABC News, ingawa bado kuna sehemu ya uvimbe bado upo, haujakuwa tena, anafanyiwa uchunguzi kila baada ya miezi mitatu, na uchunguzi mwingine umepangwa kufanyika wiki ijayo. Ingawa hakutegemea watu kuunga mkono kiasi hiko, ametoa shukrani nyingi sana.
“Inafurahisha, nafurahi kwamba nimefanya watu wengi wafahamu hili la watu wenye saratani” alisema Marshall.
Post a Comment
Powered by Blogger.