Baada Ya Watu 50 Kuuawa Nchini Marekani Donald Trump,Atoa Msimamo Wake Juu Ya Waislamu.

Donald Trump.

Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amesema mauaji ya watu 50 katika baa moja ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya Marekani.
Trump amemkashifu mpinzani wake wa chama cha republican Bi Hillary Clinton, kwa kutodadisi sababu za mtu huyo kutenda mauaji hayo.
Bi Hillary Clinton.
Upande wa Bi Clinton wakitoa risala za pole kwa waathiriwa wa mkasa huo papo hapo wamemtaja Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.
Wakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.

Fbi wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini .
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya wanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu wa aliyekuwa tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini.
Post a Comment
Powered by Blogger.