BAADA YA UCHAGUZI,MALENGO YAFUATE.

Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji.
BAADA YA UCHAGUZI, MALENGO YAFUATE.

Hatimae baada ya wiki kadhaa za kizungumkuti na malumbano kati ya Yanga kwa upande mmoja na baraza la michezo la taifa (BMT) na shirikisho la soka (TFF) kwa upande mwingine, sintofahamu hiyo imekwisha baada ya Yanga kufanya uchaguzi wake kwa amani na hatimaye kupata viongozi wake watakaoongoza kwa miaka minne ijayo.
Nichukue nafasi hii kama mdau wa soka kumpongeza mwenyekiti Yusufu Manji kwa kutetea nafasi yake hiyo tena bila kupingwa, lkn pia nimpongeze makamu wake Clement Sanga naye pia kwa kutetea nafasi yake kwa kura nyingi.
Matokeo na namna uchaguzi huo ulivyofanyika unatoa ishara juu ya imani waliyonayo wanachama kwa viongozi wao.
Baada ya kufanyika uchaguzi huu sasa ni wakati wa kuongozwa na malengo.
Wengi wametoa mawazo yao juu ya nn viongozi wapya wafanye ili kuifanya klabu iendelee nk
Kwangu mm kuna lengo moja kuu ambalo natamani kuona uongozi huu unalizingatia kwa nguvu zake zote.
Wengi wanazungumzia uwanja, mapato nk, lkn mimi niko tofauti kdg ingàwà natamani kuona hayo yote yakifanyika na Yanga hata vilabu vingine ili kupata vilabu imara na hatimaye ligi bora.
Lakini kwangu mimi lengo kuu ninalotamani kuona uongozi unahakikisha unalitimiza kwa nguvu zake zote ni kuhakikisha Yanga inazidi kuwa bora ndani ya uwanja hasa ktk michuano ya ngazi ya vilabu Afrika. Tufike mahali ambapo Yanga kucheza hatua ya makundi Afrika siyo jambo la nadra tena bali iwe ni kawaida.
Ubora wa klabu uwanjani huvuta wadhamini na wawekezaji wenye mitaji mikubwa lkn pia hii ni moja kati ya vyanzo vizuri vya mapato kwa klabu husika.
Jaribu kufikiria ikiwa kila msimu una uhakika wa kupata zaidi ya Tsh 800 mil, kwa kuingia katika hatua ya makundi na hii ni nje ya udhamini unaoweza kuupata kutokana na ubora ulionao.
Maana yake ni kwamba utakuwa na uhakika wa fedha nyingi kila msimu na kupunguza kama siyo kuondoa kbs ukata na ufinyu wa vyanzo vya mapato kwa klabu.
Sina shaka na uongozi huu kwakuwa umepata uzoefu kwa miaka ambayo wamekuwa madarakani na kufahamu vema nini wakifanye na nani wamuepuke ktk kuongoza klabu.
Wakiweza tena kutunza umoja na amani klabuni, wakiziba mianya ya uhujumu dhidi ya klabu kwenye masuala ya usajili, mishahara, kambi nk na kuzingatia weledi ktk kila hatua nategemea kuiona Yanga ya tofauti miaka mitatu ijayo.
Sitapenda kuona wajumbe wa kamati ya utendaji wanatumia vyombo vya habari kama ukumbi wa mikutano, kama kuna tofauti basi ziishie kwenye vikao vyenu ili kutunza sura ya umoja wa klabu.
Ushiriki wa Yanga ktk hatua ya makundi ya kombe la shirikisho iwe ni chachu ya kuisukuma klabu mbali zaidi.
Kila la heri uongozi uliochaguliwa macho yote yapo kwenu kuipeleka klabu kule ambako wapenda maendeleo ya soka wanaota kufika


Imani K Mbaga
0717469593

Post a Comment
Powered by Blogger.