Baada Ya Shilole Kudai Video Ya Jike Shupa Inamdhalilisha, Nuh Mziwanda Kayasema HayaNi ‘mapovu’ ‘mapovu’ ‘mapovu’, well baada ya video ya Nuh Mziwanda Jike Shupa kuwa hewani aliyewahi kuwa mpenzi wake Shilole alilazimika kuongea na kulalamikia video hiyo kuwa inamdhalilisha na kutoa utu wake kwa sababu asilimia 100 inamlenga yeye.
Nuh Mziwanda kupitia ukurasa wake wa Instagram, amemtaka Shilole kuacha kujishuku kwa sababu yeye amefanya kile anachokiona sahihi katika muziki wake.
Mkali huyo ambaye wimbo wake unaendelea kushika kasi, amedai kuwa Ex wake huyo wazamani anawapigia simu baadhi ya watu akiwataka kuacha kupost clips zozote za video yake kwakuwa inamdhalilisha.
Tazama waraka mzima wa Nuh hapo chini,
“Siku zote nilikua nataman kuwaomba sana msamaha mashabiki wangu kwa kunimiss kimuziki na kuwapa kile wanachostahili.sababu ya nilipotoka.ila nasikitika sana kwa habari ambazo mimi nakaushaga tu ila now naona ni too much ‘kama mwanaume lazma niongee ikizidi sana.ridhiki upangwa na Mungu na nawashukuru sana wanaonisapot kwenye mziki wangu ‘ila nashangaa binadam mwenzangu anadiriki kupigia sim baadhi ya mastar walionipost clip za video yangu na kuwaambia wazifute kwenye akaunti zao eti wanamdharirisha ‘jamani mbona mimi sina noma nae na nafanya muziki wangu na Mungu wangu.mpka cover yake nikapost kwa huruma ya kibinadam ambayo ninayo.mana najua siri ya mafanikio ni kuthamin kazi ya mwenzio na kutokua na chuki.haya sasa habari zote nimepata unahangaika kuishusha jike shupa ‘huwezi mana tunaishi chini ya Mungu.na huwezi zuia nguvu ya mashabiki wangu ambao wapo tayari kwa chochote kwa ajili ya muziki wangu.mangapi ya kunidharirisha umenifanyia mimi nilinyamaza mpaka wasanii wenzangu wanayajua.nimeimba kilichonitokea kwenye maisha yangu halisi na ndio siri ya muziki ni hisia na yale ambayo yanatendeka katika jamii.unasema nakudharirisha vipi wewe nlivokufumania live mbele ya wasanii wenzangu?unajua niliumiaga kiasi gani au heshima yangu ilishuka kiasi gani.Nahisi ulidhani nikitoka huko sitoendelea kimuziki.dada naamini ndani ya kipaji changu.na kingine nakushauri fanya kazi acha skendoz hazina mpango.mashabiki now wanataka mziki mzuri mana stejini hauwezi imba skendo.eti mpaka unalia kwenye sim unadharirishwa na nyimbo yangu watu waliopost wazifute wanakudharirisha mwanamke mwenzao.Mama kua na roho ya kibinadam utafanikiwa acha roho mbaya na chuki.mimi nadeal na Mungu wangu na mashabiki wangu na naamini ndani ya kipaji changu.na usipanik sana huu mwanzo tu bado Ngoma nyingi kali zinakuja.USINIPANDIKIZIE CHUKI kwa WATU nakuomba .kila mtu afanye kazi zake.samahan mashabiki zangu kwa hili mana limeniuma sana sana sio ubinadamu kabisa.na hawazifuti ng’o.Mungu yupo na mimi.pia big up kwa wale wanaokuogopa na kushindwa kunsapot kisa wewe.ila haya maisha tu na tunaishi na kufa.sasa sidhani mkisikia nimekufa mtashindwa kuja kunizika kisa bibie anapga mkwara.haya maisha jamani” Ameandika Nuh.


BONYEZA HAPA KUANGALIA HAPA VIDEO YA NUH MZIWANDA NA ALI KIBA #JIKESHUPA
Post a Comment
Powered by Blogger.