BAADA YA KUTUPWA NJE NA ICELAND KOCHA WA UINGEREZA ACHUKUA UAMUZI HUU.

ROY HODGSON ABWAGA MANYANGA ENGLAND

Kocha-England
Roy Hodgson amejiuzuluzu kama kocha mkuu wa England baada ya kikosi chake kuchezea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Iceland kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.
Kocha huyo mwenye miaka 68 amekinoa kikosi cha England kwa miaka minne akichukua nafasi ya kocha raia wa Italy Fabio Capello lakini amejikuta akishinda mechi tatu pekee kwenye mashindano makubwa ya kimataifa.
Iceland taifa lenye wakazi wasiopungua 330,000 ilikuwa ndiyo timu inayopewa nafasi ndogo zaidi kwenye michuano Ulaya inayoendelea Ufaransa.
“Samahani, inabidi nimalize kwa style hii lakini tayari yaliyotokea yametokea,” amesema Hodgson.
“Natumaini bado mtaendelea kuiona timu ya England kwenye fainali za mashindano makubwa hivi karibuni”, aliongeza.
“Kwa sasa ni wakati wa mtu mwingine kuja kuendelea na vijana wenye njaa na wenye vipaji.”
Hodgson ambaye ameshinda mechi 33 kati ya 56 akiwa madarakani, anagekuwa nje ya mkataba baada ya kumalizika kwa mashondano haya na inataarifa angeweza kuongezwa mkataba mwingeine baada ya kufanya mazungumzo na ma-boss wa FA.
Mwenyekiti wa FA Greg Dyke alishatoa kauli kwamba, Hodgson angeonezewa mkataba wake kama tu timu ingefanya vizuri Ufaransa, huku akisema angalau hatua ya robo fainali lakini walitakiwa kuifunga Iceland ili kufanikisha hilo.
Kauli iliyotolewa na FA baada ya Hodgson kujiuzulu, FA imesema: kama taifa
England ilifuzu kucheza Euro 2016 kwa rekodi ya aina yake. Walianza michuano hiyo kwa sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Russia kabla ya kuichapa Wales 2-1 na kutoka sare ya 0-0 Slovakia kwenye hatua ya makundi na kufanikiwa kufuzu kwa hatua ya 16 bora.
Chini ya Hodgson kikosi cha England, walifika hatua ya robo fainali kabla ya kuchezea kichapo na Italykwenye michuano ya Ulaya iliyopita .
Post a Comment
Powered by Blogger.