BAADA YA KUFUNGWA NA TP MAZEMBE,HAYA NDO MANENO HANS VAN DER PLUIJM KOCHA WA YANGA.

Hans Van Der Pluijm.

Kocha wa Yanga Hans van Pluijm amesema ukicheza na timu kama TP Mazembe na ukapata nafasi inabidi uitumie vizuri kufunga goli kwasababu huwezi kupata nafasi nyingi kwa timu ya aina ya Mazembe.
‘Kibabu’ amesema, timu yake ilizidiwa kwenye eneo la kiungo kutokana na viungo wake kupoteza ubora wakati wa kipindi cha pili.

“Timu yangu ilipambana sana lakini kwa bahati mbaya tukaruhusu goli kipindi cha pili, tulishindwa kutumia nafasi kama mbili au tatu tulizopata kipindi cha kwanza”, alisema Hans kwenye mkutano na waandi wa habari mara baada ya mchezo wa Yanga vs TP Mazembe kumalizika.

“Ukicheza na timu kama TP Mazembe halafu hupati nafasi nyingi, ukipata nafasi unatakiwa kuitumia kufunga, kama haufungi magoli hauwezi kushinda mechi
“Kwa upande mwingine, TP Mazembe wana  timu yenye wachezaji wenye nguvu. Tulipoteza ubora wetu kwenye eneo la kiungo.”
“Tulifanya mabadiliko lakini haikusaidia, ni sehemu ya mchezo nampongeza sana kocha wa Mazembe.”


Post a Comment
Powered by Blogger.