Hizi Ndo Mechi 6 Ambazo Hutakiwi Kuzikosa Kuzitazama EURO Hatua Ya Makundi.ITALY VS BELGIUM JUNE 13
June 13
Ni nadra sana kwa timu mbili zenye matumaini ya kutwaa kombe hili kukutana hatua ya makundi na ndiyo maana mechi hii inasubiriwa kwa hamu sana na mashabiki. Belgium wanacheza michuano yao ya kwanza ya Euro tangu mwaka 2000 na safari hii ndiyo timu namba moja inayoshiriki michuano hii.
Kocha wa Italy Antonio Conte akizungumzia mechi hii alisema “hii ndiyo mechi itayotuambia kila kitu au ndiyo mechi amabayo haitotuambia chochote”, kwa kusema  kwamba “haitotuambia chochote” anamaana kwamba itakuwa mapema sana kwenye michuano hiyo kutabiri chochote.
Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa mechi kali sana iliyoisha kwa ushindi wa Belgium 3-1 lakini haya si matokeo ya kuzingatia sana kwani Italy walikuwa wanacheza bila kiungo wao Marco Verrati na licha ya hiyo waliweza kutengeneza nafasi nyingi na walikuwa na uwezo wa kushinda mechi hiyo kirahisi. Italy walitangulia mbele kwa goli la Antonio Candreva na walipata nafasi nyingine kabla ya Jan Vertonghen kurudisha. Waliendelea kucheza vizuri ila walipigwa magoli mawili ya haraka katika dakika za mwisho ya mechi hiyo.
Tunachoweza kutoa kwenye mechi hiyo ni kwamba Italy walitumia mbinu nzuri sana na kwamba ndiyo timu yenye kocha bora zaidi kwenye pambano hili, kwani Conte kamzidi uwezo kocha wa Belgium Marc Wilmots.

AUSTRIA VS HUNGARY JUNI 14
Austria na Hungary zilikuwa himaya moja kabla ya kutengana miaka kadhaa iliyopita baada ya vita ya Dunia ya kwanza. Historia baina ya nchi hizi ilizaa upinzani mkali kwenye mpira na hii ndio mechi ya pili ya kimataifa iliyochezwa mara nyingi zaidi baada ya Argentina-Uruguay. Kati ya mechi 136 Hungary imeshinda 66 wakati Austria imeshinda 40 huku 30 zikiisha kwa droo.
Timu hizi mbili zinakutana siku ya Jumanne ikiwa imepita miaka 10 tangu mara ya mwisho zilipokutana. Austria walifungwa mechi hiyo na wachezaji wengi wa Hungary walioshinda mechi hiyo bado wanauhusiano wa aina moja au nyingine na timu yao hivi sasa tukianzia kwa Golikipa wao veteran anayevaa track-suit uwanjani Gabor Kiraly mpaka mfungaji wao siku ile Zoltan Gera
Matumaini ya wengi ni kwamba safari hii matokeo yatakuwa tofauti. Austria ni moja ya timu ambazo zinatabiriwa kufanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huu kutokana na ubabe walioonesha kwenye hatua ya kufuzu ambapo walishinda mechi 9  kati ya 10 walizocheza tena kwenye kundi ambalo lilihusisha timu za Russia na Sweden ikiongozwa na Zlatan Ibrahimovic.
Timu ya Austria inaongozwa na mchezaji wa Bayern David Alaba na nyota wa Stoke City Marko Anaurtovic na macho yote yatakuwa yanawatazama siku ya Jumanne lakini Hungary ambao wanacheza michuano mikubwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 30 watakuwa wanasubiri kwa hamu kuzima moto wao.


ICELAND VS PORTUGAL JUNI 14
June 13 1
Hivi ilikuwaje kuwaje mpaka timu ya Iceland ambayo idadi ya watu waishio nchini humo ni ndogo zaidi kushinda watu waishio wilayani Ilala Dar-es-salaam ikaweza kufuzu kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 na kumfunga Uholanzi mara mbili.
Jibu ya swali hilo ni rahisi Iceland waliweza kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye maendelezo ya vipaji vya mpira kwa vijana wao.
Chini ya Kocha Lars Lagerback Iceland ambayo ilikuwa timu namba 133 miaka minne iliopita iliweza kupanda nafasi 100 kwa sababu hii na wanaingia michuano ya Euro kama timu ndogo zaidi iliyowahi kufuzu kwenye michuano mikubwa. Unaweza kujiuliza kwamba vijana wa Iceland wanafanyia wapi mazoezi wakati nchi yao nzima imetawalia na barafu? Jibu ni kwamba serikali yao imetengeneza viwanja mbalimbali vya ndani nchi nzima na inawezekana kwamba ni viwanja hivi ambavyo nyota wao Gylfi Sigurdsson alivitumia kunoa kipaji chake.
Iceland ni timu rahisi kuishabikia Euro 2016, hata Portugal pia ikiongozwa na Cristiano Ronaldo na wengi watawasha luninga zao dunia nzima kushuhudia mechi hii.


ENGLAND VS WALES JUNI 16June 13 2
Mji wa Lens utakuwa mwenyeji kwa mechi kali sana mwaka huu. Inasemekana kuwa mamlaka ya mji huo inaogopa sana mechi hii kiasi kwamba ina mpango wa kupiga marufuku uuzaji wa vilevi siku hiyo.
Kwa kawaida England na Wales huungana kama himaya moja na watashiriki wote kuwania medali kwenye mashindano ya Olympics baadaye mwaka huu lakini kwenye mpira na Rugby hawa ni mahasimu wakubwa.
Historia inasema kama England itaibuka kidedea kwani wameweza kushinda mechi 66 kati ya 101 zilizochezwa lakini hiyo ilikuwa zamani kwani sasa Wales wanaongozwa na mchezaji Gareth Bale ambaye ana uwezo wa kuipa timu yake ushindii peke yake na ataifanya timu yake iamini kwamba kweli kumfunga England inawezekana.
Wales walimfunga Belgium kwenye hatua ya kufuzu na England wasipokuwa makini wanaweza kurudi nyumbani na majonzi. Itakuwa mara ya kwanza kwa Wales kushiriki michuano ya Euro na hakika watakuwa na hamu sana ya kumpiga kaka yao mkubwa.

GERMANY VS POLAND JUNI 16
Mechi nyingine itayopigika siku hiyohiyo ni kati ya Germany na Poland. Timu hizi mbili zitakutana kwenye uwanja mkubwa zaidi wa Euro 2016 uwanjani Stade de France. Japo Germany ndiye mbabe wa pambano hili akiwa amefungwa mechi moja tu kati ya ishirini alizocheza na Poland, usifanye makosa kufikiri kwamba Germany hamuogopi Poland.
Germany ilimtawala Poland kwenye vita ya dunia ya pili kuanzia mwaka 1939 mpaka 1945 na japo muda ni tiba ya maumivu yeyote yale lakini kidonda hiki ni kikubwa sana na ndiyo maana mashabiki wa Poland wanaisubiria mechi hii kwa hamu.
Poland ndiye waliokuwa wafungaji bora wa hatua ya makundi wakiwa wamefunga magoli 33 huku mshambuliaji wao Robert Lewandowski akiwaongoza na magoli yake 13, lakini timu hii haimtegemei yeye peke yake kwani pia kuna mshambuliaji Arkadiusz Milik ambaye aliifungia Ajax magoli 24 msimu huu na ambaye aliweza kutupia magoli 6 kwenye hatua ya kufuzu. Pia kuna winger Jakub  Blaszczykowski ambaye alishawahi kufika fainali ya ligi ya mabingwa na Borussia Dortmund, Gregorz Krychowiak kiungo maridadi wa timu ya Sevilla ambaye kashinda kombe la Europa League mara tatu mfululizo na beki Kamil Gilk ambaye ni mmoja wa mabeki bora kwenye ligi ya Serie A.
Kwenye hatua ya Kufudhu Poland aliweza kumfunga Germany katika ushindi wa 2-0 magoli ya yakifungwa na Milik na Mila.
Germany ndiye anayetabiriwa ushindi, ila hii ndiyo timu bora zaidi ambayo Poland wameweza kuipeleka kwenye michuano yeyote ile kwa miaka mingi sana na Ujerumani lazima iipe heshima yake.

CROATIA VS SPAIN JUNI 21
June 13 3
Hii ndiyo inatabiriwa kuwa mechi kali zaidi kwenye hatua ya makundi ya Euro 2016. Croatia wanaweza kwenda ana kwa ana na Spain, viungo wa Croatia ni Luka Modric anayechezea Real Madrid na Ivan Rakitic anayechezea Barcelona, kwenye safu yao ya Ushambuliaji wana Mario Mandzukic wa timu ya Juventus na atajaribu kupamabana na wakina Gerard Pique na Sergio Ramos kwenye safu ya Ulinzi ya Spain.
Pambano hili litakuwa la hali ya juu sana na litakuwa kiasharia cha uwezo wa timu hizi mbili na wapi zitaweza kufika kwenye mashindano haya. Yeyote atayemaliza kidedea kwenye kundi hili atapata njia rahisi sana hadi nusu fainali ya mashindano haya wakati atakayemaliza nafasi ya pili atapata wakati mgumu sana kutokana na jinsi mashindano haya yalivyopangwa mwaka huu.

Post a Comment
Powered by Blogger.