Angalia Kilichompata Huyu Jamaa Aliejifanya Mwanamke Na Kuwaibia Wanaume

Grace

Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanaume mmoja amabye alijitambulisha kwa jina la Grace.Grace alituhumiwa kuvaa mavazi ya kike na kuwaibia wanaume wenzake akijifanya kama yeye ni changudoa.
 Grace alikua amevalia wigi kichwani na make up ya maana usoni mwake huku akitembea kwa mwendo wa mikogo uliosababisha wanume wengine waliomuona kushawishika na muonekano wake wakidhani ni mwanamke.
 Mwanaume mmoja alifanikiwa kumtongoza Grace na kwenda nae moja kwa moja hadi kwenye Bar iliyojulikana kwa jina la Mumias. Mwanaume huyo ambae alikua tayari ameshajipanga kwa ajili ya mchezo alikwenda moja kwa moja na kulipia chumba kwenye Baa hiyo.
 Grace alianza kuonekana ni mwenye wasiwasi hali iliyopelekea mwanaume huyo aliembatana naye kumshitukia kuwa hakuwa mwanamke kama alivyodanganya bali alikua mwanaume.
Mwanaume Yule hakutaka kumuacha Grace aondoke kirahisi aliwaita kundi la wahuni wengine ili waje kumshughulikia Grace, Lakini Grace alifanikiwa kupata upenyo na kukimbilia kituo cha polisi cha jirani kwa ajili ya usalama wake.

Alishikiliwa kwa muda na bbadae aliachiwa baada ya Yule jamaa kutofika kituoni hapo kwa maelezo zaidi.
Post a Comment
Powered by Blogger.