Almanusura Ronaldinho Gaucho Ajiunge Na Manchester United.

Story By: Wilson .J. Oruma


HIVI UNAJUA KUWA ALMANUSURA RONADINHO GAUCHO AJIUNGE NA MANCHSTER UNITED?  NA HIVI INGEKUWAJE KAMA HIYO DILI INGEMILIKA HII HUWEZI KUIPATA POPOTE ISPOKUWA ALIMANUSURA.Twende sote.
Ulikuwa ni msimu wa 2003 msimu ambao ungekuwa wa kihistoria sio tu kwa man united lakini pia kwa soka la uingereza kwa ujumla. Na Japo Msimu huu man united waliuanza kama mabingwa watetezi wa EPL  lakini  kama wanasema nyota njema huonekana asubuhi basi hata nyota mbaya pia huonekana asubuhi kwani tayari Man united walishampoteza Rio Ferdinand aliyeshindwa kwenye vipimo  vya dawa za kuongeza nguvu kwa miez nane na tayari wanampoteza David Beckham kipenzi cha waingereza anayetimkia Real Madrid.
Martin Ferguson ambaye ni kaka wa Sir  Alex Fegurson ndo alikuwa na jukumu lakuhakikisha sio tu pengo la David Bekham linazibwa lakini pia Machester united wanatetea ubingwa wa Epl na bila shaka Martin alifanya zaidi ya kile sir Alex ferguson alichokitaka kuleta moja kati ya bidhaa muujarab sokoni Ronaldinho Gaucho.
Kwa PSG wao tayari wamesharuhusu dili kukamilika kwa mchezaji kukubaliana masuala binafsi na Manchester united na magazeti ya uingereza yalikuwa na vichwa vya habari kuwa ni chini ya masaa 48  Ronaldinho atakuwa amevaa jezi ya Man united na tayari baadhi ya maeneo dunian jezi ya  Gaucho ilikuwa tayari inauzwa.
Lakini ni ukweli usiopingika kuwa kama haiko mikononi mwako hata kama ni yako sio ya kwako hyo na kablya ya kukubaliana na Manchester united tayari Ronaldinho ameshazungumza na rafiki yake Sandro Rosell aliyekuwa anagombania Urais wa FC  Barcelona kuwa kama watashinda uchaguzi basi atatua Barcelona na masaa kadhaa Rosell alimjuza Ronaldinho kuwa watashinda uchaguzi na Man united wakaachwa kwenye mataa.
Lakini unashangaa kwann mchezaji anakataa kuja England kucheza moja kati ya timu tajiri duniani?unagundua kuwa pesa ni muhimu sana lakini sio kila kitu na nyumbani ni sehemu ambayo ukifika tu unakaribiswa mpaka chumbani.kwa hyo Ronaldionho alitamani sana kwenda na Spain kwani sio tu ni kama nyumbani walikopita kina Rivaldo Ronando na Romario lakini pia ni nchi inayotembelewa zaidi duniani ukiacha Ufaransa.
Kwa Wabrazil waliozoea maisha ya Copa cabana basi Cola conta ni sebuleni na Ibiza ni chumbani sintozungumzia Palma de mallorca na warembo wake na magitaa ya kispaniola.
Rakini wahenga wanasema mlango mmoja  wa mbele ukifungwa basi ujue wa nyuma unafunguliwa kwan Manchster united hawakufanikiwa sio tu kuutea ubingwa ambao ulitua mikononi mwa Arsenal tena bila kufungwa walimkosa Ronaldionho lakini walifanikiwa kumsajili Christiano Ronaldo aliyewapa taji la UEFA Champions league na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia msimu wa 2008.
Ronaldinho mwenyewe alienda FC BARCELONA na kuichezea michezo 207 akiifungia magoli 94  na kusaidia mengine 69 yaliyopelekea kutwa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mara mbili mfululizo 2004 na 2005.
Alizaliwa tarehe 21 march 1980  Bandarini Porte Alegre na wazazi Dona Miguelina na baba  Joao De Assis Moreirra wazazi wake wakamuita Ronaldo De ASSIS MOREIRA  lakini kutokana na kuwa mdogo sana uwanjani wenzake wakabatiza Ronaldinho.
Alianza mapenzi yake na soka kwa kucheza sana beach na mpira wa ndani maarufu sana Brazilil kama FUTSAL Mchezo ambao umewatoa wanasoka wengi sana nchini Brazil.Alianza kucheza soka na Timu ya Gremio na baadae akijiunga na PSG msimu wa 2001 akicheza sambamba na Nikolas Anelka na Austine jay jay Okocha.
Na dunia imemfahamu sana kuwa uwezo mkubwa wa chenga zisizomithirika,Ufundi usiopimika,pasi za bila kutazama na uwezo mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa au free kicks.

Post a Comment
Powered by Blogger.