Al-Shabab Wasema Wamewaua Wanajeshi 40 Nchini Ethiopia.


Wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini Somalia wanasema kuwa wamewaua wanajeshi 40 wa Ethiopia katika kambi ya Umoja wa Afrika katikati ya Somalia.
Wakaazi wa Halgan wameiambia BBC kwamba walisikia mlipuko mkubwa uliofuatiwa na ufyatulianaji wa risasi.
Umoja wa Afrika Amisom umethibitisha kuhusu shambulio hilo lakini unasema lilikabiliwa vilivyo.
Amisom inaunga mkono serikali ya Somalia huku ikitafuta kulidhibiti taifa hilo kutoka kwa mikono ya wapiganaji wa al-Shabab.
Katika misururu ya ujumbe wa Tweeter Amisom imesema kuwa wanajeshi wake wakisaidiwa na wale wa Somalia waliwafurusha washambuliaji hao ambao sasa wametoroka huku wakisakwa na wanajeshi wa Amisom.
Post a Comment
Powered by Blogger.