Airtel Yakiwezesha Chuo Cha Taifa Cha Utalii (NCT)


Katika kuendeleza dhamira ya kusaidia Jamii kwa kujenga ubora wa ya elimu ya ICT hapa nchini,Kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel imekabidhi kompyuta 30 kwa Chuo cha utalii cha Taifa (NCT) ambapo ni sehemu mojawapo ya mipango yake ya kusaidia vijana wajasiriamali hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA wa kutoa huduma kwa jamii katika kuboresha upatikanaji wa teknolojia ya kisasa na ubora wa elimu nchini Tanzania.
Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia) akizungumza na vyombo vya habari wakati wa hafla ya makabidhiano ya kompyuta 30 kwa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja Msaidizi wa chuo Oscar Mwambene (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kushoto), hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.
 Mkuu wa idara ya Utalii katika Chuo cha Taifa cha Utalii Elina Makanja (Kushoto) akimwelekeza mwanafunzi Agape Gerald (Kulia) mara baada ya kukabidhiwa kompyuta 30 kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Katikati)

 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) wakitumia kompyuta zilizokabidhiwa na Airtel kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa.

Post a Comment
Powered by Blogger.