AbduKiba Afungukia Ishu Ya Kufanya Kazi Na WCB Wasafi

Abdukiba
 Msanii Abdukiba ambaye ni mdogo wa Alikiba amefunguka na kusema kama ikitokea WCB Wasafi wakataka kufanya kazi na yeye inawezekana kwani yeye anaangalia mpunga (pesa) zaidi,
hivyo kama watakuwa na pesa za kutosha na makubaliano mazuri anaweza kufanya kazi chini la Label hiyo ya 'WCB Wasafi'
Abdukiba amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio baada ya moja ya shabiki kutaka kufahamu kama ikitokea WCB wakiataka kufanya naye kazi atakuwa tayari? ndipo hapo aliposema yeye anaangalia pesa hivyo kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya naye kazi anaweza kufanya kazi chini la label hiyo ya WCB Wasafi.
Mbali na hilo msanii huyo amesema kuwa Kiba Square inarudi muda si mrefu kutoka sasa kwani zilikuwa zinasubiriwa kazi ya Alikiba 'Aje' pamoja na hii kazi yake yeye mpya 'Bayoyo' ila baada ya hapo ndipo project zile za Kiba Square zitakuja.

Angalia Hii Ya Rapper Young Killer Akiongelea Ishu Ya Kujiunga WCB

Post a Comment
Powered by Blogger.