ABDALLAH HAMISS:LULU ILIYOJIFICHA NA KUNG^AA NJE YA MIPAKA.

Abdallah Hamiss.

ABDALLAH HAMISS: LULU ILIYOJIFICHA NA KUNG'AA NJE YA MIPAKA.

Jioni hii ya leo michuano ya top 8 pale Kenya itafikia kilele kwa mchuano kati ya Gormahia na Muhoroni.

Wakati tukielekea kwenye mechi hii jicho langu linamuangukia kijana kutoka Tarime, kwa jina la ABDALAH HAMIS akicheza nafasi ya kiungo mkabaji, huku akiwa na umri wa miaka 23 tu, aliweza kuvuka mpaka na moja kwa moja kuanza kuichezea klabu ya Muhoroni.


DULLA kama ninavyopenda kumuita, alianzia soka lake nyumbani kwao kule Tarime akizichezea timu za Tarime Utd na Tarime Wor, kabla ya kutimkia Stand Utd na kuisaidia kupanda daraja.
Baada ya hapo Dullah aliingia nchini Kenya na kuanza kuchezea kikosi cha vijana cha Muhoroni kabla ya kupata nafasi ktk kikosi cha kwanza cha wakubwa.


Kabla sijamfuatilia vizuri licha ya kujua kuwa ni mchezaji tokea kule Tarime, nikaliona jina lake likitokea katika ubao wa magoli "Score board" juma lililopita akiifungia timu yake ya Muhoroni goli dhidi ya Ulinzi Stars ktk mchezo uliokwisha kwa matokeo ya 1-1 na goli lake hilo kuipeleka timu yake kucheza fainali dhidi ya Gor leo jioni.
Nilipofanya naye mahojiano wiki iliyopita Dullah aliniambia kwa furaha,


"Nafurahi sana kupata nafasi ktk kikosi cha kwanza, mwalimu ananiamini na kunifanya nijiamini, naamini ipo siku nitachezea timu yangu ya taifa" alisema.


Moja kati ya nafasi adhimu ktk mpira wa kisasa ni nafasi ya kiungo mkabaji anayoichezea Dullah.
Ninapoona mchezaji anayechezea klabu yoyote ile anapata nafasi ya kudumu ktk kikosi cha kwanza ktk nafasi ya kiungo mkabaji huwa naamini kuwa ana kitu fulani cha ziada.


Kazi ya kulinda walinzi, "ku-block" mashambulizi ya maadui, kuanzisha mashambulizi nk, hii unahitaji mtu makini, imara kimwili na kiakili, mwenye mtazamo wa mbali na mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu.


ABDALLAH HAMIS licha ya umri lkn kimo chake pia vinamfanya kuwa lulu iliyofichika na kung'aa nje ya mipaka.
Tayari kuna taarifa kuwa klabu ya Sofapaka kutoka kule kule nchini Kenya inahitaji huduma yake ingawa mwenyewe hakuwa tayari kulizungumzia hilo lkn naamini siku zote muda utaongea
Huyo ndiye ABDALLAH HAMIS lulu iliyofichika inayong'aa nje ya mipaka.                            Imani K Mbaga                            0717469593
Post a Comment
Powered by Blogger.