Yanga Yaibugiza Ndi Ndi Mbeya City Sokoine Na Kukabidhiwa Kombe Jumamosi Taifa Dhidi Ya Ndanda.

Yanga.
Wakicheza katika uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya dhidi ya timu ya Mbeya City katika mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara na mchezo umemalizika kwa Yanga kushinda 2-0.
Mbeya City.
Mchezo ulianza kwa kasi na kushambuliana mnamo dakika ya 8 kipindi cha pili Yanga walipata pigo kwa kiungo wao mkabaji kuumia vibaya Mbuyu Twite na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Telela.
Mbuyu Twite.
Dakika ya 25 Yanga waliandika bao moja kupitia kwa baki kisika Vicent Bosou kwa kichwa akiunganisha corne iliyochungwa na Simon Msuva na katika dakika ya 32 Vicent Bossou aliumia vibaya baada ya kugongana na Kenny Ally na kupelekewa kutolewa kwa machela huku akiwa katika hali mbaya na nafasi yake ilichukuliwa na Kelvin Yondani hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Vicent Bossou.
Kipindi cha pili kilianza kwa wenyeji kulishambulia lango la Yanga huku kipa Ally Mustaph akifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo dakika ya 21 Donald Ngoma alikosa bao la wazi baada ya uzembe wa mabeki wa Mbeya City.
Dakika ya 86 Amis Tambwe alifunga bao la pili na likiwa bao lake la 21 na kumuacha Hamis Kiiza Wa Simba akibaki na mabao 19 na Jumamosi hii watakabidhiwa kombe lao la ubingwa kwani wamefikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yote na mchezo wa dhidi ya Ndanda utachezwa uwanja wa Taifa badala ya kuchezwa mtwara kutokana na uongozi wa Ndanda na Yanga wamekubaliana .
Hamis Tambwe.

Juma Kaseja.
Post a Comment
Powered by Blogger.