Hassan Kessy Wa Simba Asaini Yanga Mkataba Miaka 2.

Hassan Kessy.
Hatimaye imejulikana mchezaji aliyesimamaishwa na klabu Ya Simba Hassana Kessy wiki chache zilizopita kwa utovu wa nidhamu kwa madai ya kucheza rafu ya makusudi kwa mchezaji wa Toto Africa na timu yake ilifungwa 1-0.
Kessy amechukua uamzi mgumu kwa kusaini mkataba wa awali na timu yaYanga ambao ni watani wa jadi huku akiwa amesimamishwa na klabu yake huku mkataba wake unaelekea kumalizika mwezi huu.
Beki huyu kisiki aliyeitengenezea mabao mengi klabu ya Simba msimu huu inadaiwa kuwa usajili wake wa miaka miwili wa kujiunga na mabingwa watetezi wa Vodacom ligi unatajwa kuwa ni pesa nyingi sana ikiwemo na kupewa gari na nyumba na anatajiunga na klabu yake mpya mwezi wa sita.
Post a Comment
Powered by Blogger.