Yanga Kuwakosa Ngoma Na Kamusoko Leo Dhidi Ya Waangola Huku Hans Van De Pluijm Akitoa Tamko.

Kocha wa Yanga akiwa na Ngoma na Kamusoko.
Klabu ya Yanga kuelekea mchezo wake wa kombe la shirikisho dhidi ya timu ya Sagrada Esparanca ya Angola utakaochezwa  katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imepata pigo kwa wachezaji wake muhimu wa kimataifa kutoka Zimbambwe kuukosa mchezo huu kutokana na kuwa na kadi mbili za njano Kamusoko na Ngoma hawatacheza.
Thabani Kamusoko akichuana na mchezaji wa JKT Ruvu.
Donald Ngoma akishangilia bao.
Kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo HansVan De Pluijm amesema kuwa ni kweli atawakosa wachezaji hao ila anajua wachezaji gani wataziba mapengo hayo na kusisitiza kuwa leo lazima wangola wafe Taifa kwani anawachezaji wazuri na wakati wowote watampa matokeo na kusema kuwa hata mechi ya marudiano watakuwa na kikosi kizima na kwa sababu mchezo wa leo hawatamjua Kamusoko na Ngoma hao ndo wataenda kuwasumbua huko kwao.
Kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.

Post a Comment
Powered by Blogger.