Yanga Kuukaribia Ubingwa Leo? Mjini Shinyanga Huku Stand United Mtafaruko Waendelea.

Yanga.
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara katika mzunguko wa 27 kuendelea tena leo kwa mechi moja kuchezwa katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wenyeji timu ya Stand United watawaalika vinara wa ligi hiyo timu Yanga.
Mchezo huu unatazamiwa kuwa na upinzani kwa kila timu hasa kwa wanajangwani ambao wapo katika hatua ya kutetea ubingwa wao kwa kutaka kuwafunga Wenyeji ili waweze kujiongezea pointi kwani kwenye michezo yao minne wanahitaji pointi saba ili wawaze kutwaa ubingwa kwa mara ya pili.
Stand United.
Timu ya Stand United ambao kwa sasa wapo katika mgogoro na wachezaji wake ambao wamefikia hatua ya kusimamishwa kwa mwezi mmoja na kocha mkuu wa timu hiyo wachezaji hao ni Haruna Chanongo,Abuu Ubwa na Zahiri Rajabu kila kukicha timu hii imekuwa na mzozo kwa wachezaji na kocha na viongozi kwa viongozi.
Tangu Stand wapande ligi kuu hawajawahi kumfunga Yanga na tunatarajia kuwa tutaona mpira wa ufundi na si kwa kukamiana.
Post a Comment
Powered by Blogger.