Wizara Ya Afya Imepokea Msaada Kutoka Kwenye Shirika La Duniani[ WHO].
Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi
bilioni 1.4 kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akiongea na waandishi wa habari Wizarani hapo, Mkurugenzi wa Huduma za kinga Dkt.Neema Rusibimayila ameeleza kuwa vifaa tiba vitasaidia uhifadhi wa chanjo katika mikoa mbalimbali pamoja na hslmashauri hapa nchini.

Dkt.Neema Rusibimayila.

‘’Ni msaada mkubwa tulioupata toka WHO na nina amini kuwa utatusaidia sana katika kufanikisha suala la chanjo kwa akina mama na watoto ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea''alisema Dkt.Rusibimayila.


Akikabidhi vifaa hivyo Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro
Chatoro amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 pamoja na majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa ajili ya kutolea chanjo.
Kwa upande wake Mratibu Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana Emmanuel Yohana ameeleza kuwa majokofu hayo pia yatapelekwa katika wilaya ambazo zina upungufu wa majokofu pamoja na vituo vipya kwa ajili ya kupunguza umbali kwa wagonjwa wa chanjo na pia ni moja ya kuweka huduma karibu na wananchi.


Post a Comment
Powered by Blogger.