Vilabu Mmekubali Kuendelea Na Bodi Hii Ya Ligi?.


VILABU MMEKUBALI KUENDELEA NA BODI HII YA LIGI?
Tumemaliza ligi za ndani na nje, sasa wapenda soka tunageukia michuano ya "EURO" kuendelea kuburudika na soka.
Lakini bila shaka hatuwezi kuacha kujadili yanayoihusu ligi yetu hata kama hatupati majibu leo basi historia itatuhukumu na kututetea.
Kulikuwa na mpango hapa wa kuifanya ligi yetu kuwa chini ya chombo huru ili shirikisho letu la soka libaki kushughulikia masuala ya utawala na timu za taifa.
Vilabu vya ligi kuu vilikaa na kutafuta wataalamu toka ndani na nje ya nchi ili kufundishwa juu ya hili.
Kama ilivyo kawaida TFF walikuja juu kukemea hilo na kuunda kamati ya ligi iliyo chini yake ambayo watendaji wanateuliwa na shirikisho huku vilabu vikiwakilishwa na wajumbe kutoka timu zinashika nafasi nne za juu baada ya ligi kukamilika.
Vilabu vilipokuwa na lengo la kuanzisha chombo huru kinachosimamia ligi kusudi lao kubwa ilikuwa ni kuelekea kwenye ligi ya kkulipwa kwa maana ya kupata chombo watakacho kisimamia wao wenyewe na chombo hicho kusimamia maslahi ya vilabu.
Ndoto ya kuwa na chombo hiki imezimwa kbs na shirikisho kwakuwa chombo hicho kingehatarisha maslahi binaafsi ya watu wachache wanaofaidi matunda ya soka letu.
Viongozi wa vilabu vyetu wanasumbuliwa na tatizo la ubinafsi, kutoelewa na wakati nwingine njaa binafsi hvyo hawawezi kujisimamia na kuyasimamia malengo yao. TFF wanajua udhaifu huo wa viongozi wetu na hvy kuutumia kukandamiza vilabu.
Sijawahi kuona vilabu vyetu vikiwa na kauli moja au mapatano kwa maslahi yao wakayasimamia kwa umoja.
Kila klabu "inakufa kivyake" linapokuja suala la maslahi yake bila msaada wala umoja hvy dhana ya mwenye nguvu mpishe hujihidhirisha kila wakati.
Katika misimu mingi tunaona wanaofaidika ni wale wanaoweza kumweka kiongozi pale TFF kati ya Simba au Yanga jambo ambalo halina afya kwa soka letu.
Vilabu vinasahau kwamba wao ndo wenye mpira wao na kwamba ligi ni bidhaa inayonunulika kuliko bidhaa nyingi duniani.
Vilabu vinahanggaika kuandaa timu zao kwa mateso na ugumu wa hali ya juu lkn ni kwa hasara maana wanawekeza kuboresha bidhaa "ligi" kisha wanaofaidika ni wale ambao hawakutoka jasho kabisa.
Mnataka hili muelezwe na nani ikiwa ninyi ndiyo wahusika wakuu ktk suala hili?
Kinachoshangaza bodi ya ligi tuliyonayo inaonekana kwenye upangaji ratiba ambako wameshindwa kbs kufanya hili kwa ufanisi, lakini pia tunawaona kwenyehukumu za ajabu ajabu ambazo pia nyuma yake wapo wanaoshinikiza.
Vilabu fahamuni kuwa suala la kuiuza bidhaa "ligi" ni la kwenu, bodi yenu huru mtakayoiunda ndiyo itakayokuwa na jukumu la kuhakikisha maslahi yenu ktk mikataba mbali mbali ya udhamini ambacho ndo kiini cha faida ya uwekezaji wenu.
Leo hii mnalalamika juu ya ukosefu wa fedha , vifaa duni, ucheleweshwaji wa fedha za udhamini nk lakini nani atasimamia maslahi yenu kwa uchungu kama siyo bodi mtakayoizaa wenyewe?
Hebu tufike mbali muanze kushiirikiana ktk mambo ya msingi na muhasimiane uwanjani kutupa burudani.
Mmewahi kujiuliza meneja masoko wa shirikisho ana kazi gani hasa? Anauza bidhaa gani pale? Mnawaacha TFF wanagawana vyeo na kkulipana mishahara bila jasho huku ninyi mkihangaika kulipa madeni ya vilabu vyenu.
Jambo la kusikitisha ni kwamba ukitaka kudhamini ligi ya Tanzania ni suala la kukubalika na TFF tu hata kama vilabu havikutaki bado havina nguvu ya kupinga wala kujiridhisha kwakuwa havina mkono ktk hilo
Bado najiuliza vilabu vyetu vinajua kwamba ligi wanayocheza ni bidhaa inayotafuttwa? Na je! mnafahamu kuwa kuna watu wanaofaidika na hiyo bidhaa?
Mwisho mna mpango gani sasa wa kuwa na bodi yenu kama ilivyo A Kusini au Uingereza?
Mkizubaa ule msemo wa wajinga ndiyo waliwao utawatafuna na kuendelea kulidumaza soka letu.


Imani K Mbaga.
 0717469593
Post a Comment
Powered by Blogger.