Video | Wabunge Kambi Ya Upinzani Watangaza Kutokua Na Imani Na Naibu Spika

  Kambi ya Upinzani Bungeni imetangaza kutokuwa na imani na Naibu Spika wa Bunge DK TULIA AKSON kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni na akiwabana wabunge wa upinzani kuweza kuwasilisha hoja zao ipasavyo. Tamko hilo la Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni FREEMAN MBOWE limefuatia uamuzi wa Naibu Spika wa Bunge kuwatoa nje wabunge wote wa kambi ya upinzani baada ya kukaidi agizo la kukaa chini alilolitoa baada a Mbunge wa Kibamba JOHN MNYIKA kusimama. Mnyika alisimama ili kushinikiza bunge kujadili kwanza hoja ya wanafunzi wa Ualimu wa Sayansi UDOM kurudishwa makwao kutokana na mgomo wa walimu. Baada ya kutoka nje MBOWE akaitisha kikao na kutoa maazimio.
Post a Comment
Powered by Blogger.