VIDEO | Binti Mtanzania Aliyehutubia Mkutano Wa UN Kayasema Haya Bungeni

  Machi 20 mwaka huu Tanzania na nchi zingine za Afrika Mashariki ziliingia kwenye sintofahamu baada ya kudaiwa joto kufikia nyuzijoto 40 jambo ambalo lilikanushwa na mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA.
 Hata hivyo ukweli uko palepale kwamba uharibifu wa mazingira umechangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia nchi hapa nchini, ambapo Mwanaharakati Kijana wa Mazingira ambaye hivi karibuni ameliwakilisha taifa kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akiwa Bungeni akatoa hoja. Licha ya harakati zake za kuhamasisha jamii kutunza na kulinda mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi GETRUDA akabainisha changamoto anayoiona. 
Baada ya hoja hiyo Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kutaja mkakati wake.
  Bunge linaendelea na majadiliano ya bajeti hiyo tayari kwa kuipitishe, wananchi tutunze mazingira ili yatutunze.
Post a Comment
Powered by Blogger.