Usipitwe Na Hii Makala Ina Ujumbe Mzito,USIACHE YALIYOPITA YAKAZUIA USIONE YAJAYO.

USIACHE YALIYOPITA YAKAZUIA USIONE YAJAYO.
Akili ya mwanadamu pamoja na mambo mengine, pia inahusika ktk kutunza kumbukumbu.

 Ndiyo maana yale uliyoyapitia yawe mema au mabaya yamebaki kwa kiasi kikubwa ktk akili yako.
Hali hii ndiyo inayotufanya tuweze au tushindwe kusamehe wengine wanapotukosea, na kuendelea kuwashikilia mioyoni mwetu. 


Kuwa na kumbukumbu siyo dhambi wala siyo kosa, tatizo ni hiyo kumbukumbu inakusukuma kufanya nini?
Ni rahisi sana kusamehewa na Mungu tunapomkosea na kumuomba msamaha kwa njia ya toba ya kweli lakini ni ngumu sana KUJISAMEHE.
Kujisamehe ni hatua tunayopaswa kuichukua baada ya kupitia madhila fulani yanayotusukuma kufanya makosa ktk maisha yetu.
Inawezekana unajutia maamuzi ya kuwa na uhusiano na mtu fulani, aliyekusababishia maumivu na vidonda ktk maisha yako, labda unajutia kazi, biashara, masomo, lugha, tendo au jambo lolote ulilolifanyia uamuzi na uamuzi huo ukakugharimu.
Kujuta ni hali ya kawaida inayotusaidia kufanya toba kwa Muumba na kuwaomba msamaha tuliiowakosea, lkn baada ya hapo maisha yanatakiwa yaendelee.
Hapo ndipo kwenye umuhimu wa kujisamehe kwa yale uliyoyafanya ili uipe nafsi yako uhuru na amani.
Jitahidi sana kuliepuka neno "ninge... " kila wakati ili uweze kuwa na furaha na hatimaye kusonga mbele.
Inawezekana hata unaposoma andiko hili yapo mambo unayojilaumu nayo kwa miaka kadhaa sasa. Kujilaumu huko ni dalili ya kutojisamehe na kujiweka chini ya kitanzi kinachokufanya ushindwe kuwa na furaha na amani hata pale unapofanikiwa.
Acha kuyashikilia makosa yako, kubaliana na nafsi yako kusonga mbele na kuyafanya yaliyopita kuwa yamepita.
Kuutojjisamehe na majuto yaliyopitiliza hutufanya tushindwe kuona mafanikio yetu ya mbele.
Unashindwa kuona mahusiano mapya kwa sababu ya yaliyopita, huoni rafiki mpya, huoni kazi mpya, huoni maisha mapya nk
Unajikuta huoni furaha mpya, na unashindwa kumshukuru Mungu kwa kuwa huoni yote ssliyokufanyia baada ya hapo kwa kuyashikilia yaliyopita
Kkumbuka tu "yaliyopita si ndwele.... "
Siku njema.

Imani K Mbaga.

0717-469593
Post a Comment
Powered by Blogger.