Ufahamu Ukubwa Wa Uwanja Wenye Viwango Vya Kimataifa.


Uwanja wa mpira.www.seetheafrica.comWapenzi, wachezaji na mashabiki wanaopenda mpira wa miguu bila shaka watapenda kujua ni uwanja gani  wenye vipimo vipi ambao nisahihi ka ajili ya kuchezea mpira wa miguu? na ni namna gani wachezaji wanatakiwa kujipanga ili kuleta ladha kamilini yamchezo huo unaopendwa na idadi kubwa ya watu duniani kwote kwa karne ya21
Ili uwanja uwe na sifa kamili na uliokidhi viwango vya kuchezea soka unatakiwa uwe na mambo makuu yafuatayo:
Umbo la uwanja

Uwanja una umbo la mstatili. Hakuna kipimo kamili kanuni zinasema urefu ni baina mita 90 na 120, upana baina mita 45 na 90. Kwa michezo ya kimataifa urefu uwe baina mita 100 - 110 na upana baina mita 64 na 75.

Goli ziko kwenye pande fupi zaidi. Kuna alama ya bendera kwenye kona za uwanja. Mwaka 2008 IFAB ilijaribu kusanifisha vipimo kuwa mita 105 kwa 68 lakini kanuni hii ilipumzishwa baadaye. Mstari ni mpaka wa uwanja. Wakati mpira uko kwenye mstari hata kwa kiasi kidogo unahesabiwa bado uko ndani ya wanja. Kwa goli kukubaliwa sharti mpira umepita mstari wa goli kabisa.
 
Mpangilio wa wachezaji

Kuna wachezaji wa aina tatu: Walinzi, wachezaji wa kiungo na wachezaji wa mbele au straika. Goli kipa au mlinda lango ni mmoja kati ya walinzi.

Ni uamuzi wa kocha kuhusu idadi ya wachezaji wanaocheza kuwa walinda lango, wa kiungo au wa mbele, ikitegemea mfumo uliotumika. Japo mfumo wa 4-4-2 umekuwa maarufu miongoni mwa timu nyingi. Mfumo huu hujumlisha walinzi wanne pamoja na mlinda lango, wachezaji wanne wa kiungo na wawili wa mbele.
Lakini ipo mifumo mingine inayotumika sana kwa nyakati hizi kama vile 3-5-2  yaani walinzi watatu, viungo watano pamoja na washambuliaji wawili kwa kawaida mfumo huu ni wa kujilinda zaidi. Ipo pia mifumo mingine kama vile 4-3-3,  4-1-4-1, 4-2-3-1 na mingine mingi kulinganana kocha anavyotaka timu yake icheze ili kujipatia aina fuilani ya ushindi anaouhitaji kwa wakati huo.

Kocha huamua kuweka aina fulani ya mfumo ili kujiletea matokeo kulingana na timu atakayokutana nayo, endapo atataka timu yake ijilinde zaidi basi ni dhahiri atatumia mfumo wa 4-5-1 yaani walinzi wanne, viungo watano na mshambuliaji mmoja. Hii inamaanisha viungo watacheza zaaid katikati ili kuwadhibiti wapinzani wasipate mpenyoi kirahisi.
Post a Comment
Powered by Blogger.