TPA Yasema Maneno Haya Kuhusiana Na Bandari Ya Dar es salaam.Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imeandaa mradi utakaogharimu dola 690  kwa ajili ya kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ili kukabiliana na  ongezeko la shehena ya mizigo.
Akizungumza na  Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TPA) Aloyce Matei amesema miradi itakayotekelezwa ni pamoja na uongezaji wa kina kufikia mita 14 kutoka tisa za sasa katika gati namba moja hadi saba ili kuwezesha meli kubwa kutia nanga.Alisema kuwa Benki ya Dunia kupitia Mfuko wa International Bank for Reconstruction (IBRD) itatoa mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola milioni 600.
 DFID watoa ruzuku dola milioni 30 na serikali kupitia Mamlaka ya Bandari itachangia dola milioni 60.
Maboresho mengine ni  kuongeza kina katika gati namba nane hadi 11 zilizokodishwa kwa TICTS ili kuwezesha meli kubwa kutia nanga, kujenga gati mpya ya kushushia magari katika eneo la Gerezani Creek, ufungaji wa conveyor system na ujenzi wa maghala ya kuhifadhia nafaka.Ujenzi wa gati namba 13 na 14, uhamishaji wa gati la mafuta la KOJ pamoja na uhamishaji wa mabomba ya mafuta katika eneo la ujenzi na uboreshaji wa mtandao wa reli ndani ya bandari na ujenzi wa sehemu ya kupakilia na kushushia mizigo kwenye mabehewa.
Post a Comment
Powered by Blogger.