ZijueTimu Zilizofuzu Hatua Ya Makundi Kombe La Shirikisho Africa CAF Huku Sura Za Waarabu Zikiongoza.

Michuana ya 16 ya kombe la shirikisho imemalizika jana na hatimaye timu nane zilizoingia hatua ya makundi zimejulikana huku kukiwa na sura mpya katika michuano hiyo tazama timu zilizofuzu.
Yanga.
Klabu ya Yanga Ya Tanzania imefuzu kwa mara ya kwanza katika hatua hii ya hatua ya makundi ilikuwa ligi ya mabingwa ilitolewa na Al-Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2 hivyo kuangukia katika hatua ya Shirikisho na ilikutana na Sagrada Esparanc ya Angola mchezo wa awali Yanga waliibuka na ushindi wa 2-0 na mchezo wa pili Sagrada walishinda bao 1-0 na Yanga kutinga hatua ya makundi kwa idadi ya 2-1.
TP Mazembe.
Hawa TP Mazembe toka DR walikuwa mabingwa wa kombe la ligi ya Mabingwa walivuliwa ubingwa huo na kushuka mpaka kombe la Shirikisho na walicheza na Stade Gabesien toka Tunisia na mchezo wa awali TP Mazenbe walishinda 1-0 na mchezo wa marudiano Gabesien walishinda 2-1 hivyo ikawa sare ya 2-2 na Mazembe walisonga mbele kwa faida ya bao la Ugenini.
Etoile Du Sahel.
Timu ya Etoile Du Sahel toka nchini Tunisia hawa ndo mabingwa watetezi wa kombe hili nao walikuwa katika michuano ya ligi ya Mabingwa na walitolewa na Enyimba ya Nigeria na kuweza kuingia kombe la shirikisho na waliweza kukutana timu ya Mounana toka Gabon na mchezo wa kwanza Etoile walishinda 2-0 na mchezo wa pili Mounana walishinda 1-0 hivyo Etoile wamesonga mbele kwa jumla ya 2-1.Al-Ahli Tripoli.
Mabingwa wa ligi kuu ya Libya nao walikuwa ligi ya mabingwa na walitolewa katika michuano hiyo na kuingia huku na walikutana na timu ya Misr-Marrakech toka Misri na mchezo wa awali ulichezwa Libya na timu hizi zilitoka sare ya 0-0 na mchezo wa pili timu hizi zilitoka sare ya 1-1 hivyo Tripoli wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini.
Mo Bejaia.

Hii ni timu inayotoka Algeria, Mo Bejaia na ilikuwa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa na ilitolewa na kuingia 16 bora na ilipangwa na wababe wa Azam timu ya Esperance Du Tunis na mchezo wa awali timu hizi zilitoka sare ya 0-0 na mchezo wa pili timu hizi zilitoka sare 1-1 hivyo Mo Bejaia wamesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.
Medeama SC.
Hawa  Medeama SC toka nchini Ghana waliingia 16 bora ya shirikisho na walipangwa na timu iliyotoka ligi ya mabingwa Mamelodi Sundowns mchezo wa kwanza Sundowns walishinda bao 3-1 na mchezo wa pili Medeama walishinda 2-0 na kusomeka 3-3 hivyo Medeama wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini.
Kwakaba De Marrakech.
Kwakaba De Marrakech hii inatoka Morocco na iliingia 16 ya kombe la shirikisho na walikutana na timu iliyotoka ligi ya Mabingwa timu ya Al-Merrikh toka Sudan mchezo wa awali Al-Merrikh waliibuka na ushindi wa 1-0 na mchezo wa pili Kwakaba walishinda 2-0 hivyo Kwakaba De Marrakech wamefuzu kwa idadi ya mabao 2-1.
Fus Rabat.
Timu ya Fus Rabat toka Morocco waliingia 16 na hivyo walipangwa kucheza na timu ya Stade Malien Bamako Ya Mali na mchezo wa awali timu hizi zilitoka sare ya 0-0 na mchezo wa marudio Fus Rabat walishinda 4-0 na kusonga mbele kwa idadi ya 4-0.

Post a Comment
Powered by Blogger.