Tazama Picha Za Maandamano Ya Kumpinga Rais Kabila Yafanyika Nchini DRC.
Maandamano hayo yamepigwa
marufuku katika maeneo mengine ikiwemo mji wa Lubumbashi nyumbani kwa
mgombea wa urais wa Upinzani Moise Katumbi.
Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi kuwa mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma ujumbe wa Twitter kwamba jeshi limekuwa likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.
Mwandishi huru wa habari Ley Uwara alituma ujumbe wa Twitter kwa lugha ya Ufaransa kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi watu wameshindwa kwenda kazini.
Mjini Goma katika eneo la Birere,amesema kuwa ni
mchezo wa paka na panya ambapo vijana wamekuwa wakijibizana na polisi
kwa kuwarushia mawe huku nao maafisa hao wakiwatupia vitoa machozi.
Anasema kuwa baadhi ya vijana wamekamatwa na jeshi kutumwa ili kuwasaidia maafisa wa polisi.