Tazama Picha 8 Za Bomoabomoa Ilivyoanza Leo Asubuhi Baada Ya Maafa Ya Ghorofa.

Serikali ya jimbo la Nairobi imeanza kubomoa nyumba ambazo maafisa wanasema hazifai kuishi watu.
Shughuli hiyo inatekelezwa baada ya jumba moja la makazi la ghorofa sita kuporomoka Ijumaa wiki iliyopita na kuua watu 36.
Watu karibu 70 bado hawajulikani walipo huku shughuli ya leo ni kulenga nyumba nane ambazo zimekuwa zikikaliwa na watu zaidi ya 600.
Watu wakitoa vitu vya nje.
Nyumba ambazo zimepangiwa kubomolewa zimewekwa alama ukutani.

Watu waliagizwa wahame kutoka kwenye nyumba hizo wiki moja iliyopita hata hivyo walipuuzia mpaka leo asubuhi walikuwa bado hawajahama.

Baadhi wamekuwa wakijaribio kuokoa mali yao mapema leo.

Baadhi ya wakazi wamelalamika kwamba hawana kwa kwenda.
Post a Comment
Powered by Blogger.