Tazama Jinsi Yanga Ilivyoibugiza Vikombe Vitatu Kambarage Stand United Na Azam Kunyoa au Kusuka Leo?

Yanga.
Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea jana kwa mechi moja ilichezwa katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga mabingwa watetezi wa ligi Yanga wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutetea kombe hilo baada ya kuibuka na ushindi mno wa 3-1 dhidi ya Stand United.
Donald Ngoma.
Mchezo ulianza kwa kasi huku Yanga wakitafuta bao la mapema kunako dakika ya 2 Donald Ngoma aliandikia timu yake akitumia uzembe wa mabeki wa Stand huku wenyeji walianza kulisakama lango la wageni kama nyuki dakika ya 44 Ngoma alirudi tena kwenye nyanu za Stand.
Hadi mapumzi timu hizo zinaenda ubao ukiwa unasomeka kuwa Yanga 2-0 Stand hawajapata kitu na kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kwa upande wa wageni Salum Telela alitoka na kumuigiza Mbuyu Twite dakika ya 54 Amis Tambwe anaifungia bao la tatu timu yake na likiwa la 20 katika ligi msimu huu.
Amis Tambwe.
Hata hivyo licha ya kufungwa mabao 3-0 timu ya Stand haikukata tamaa ilicheza kwa kushambulia huku ikiwa haina malengo kwa washambuliaji wake kukosa umakini dakika ya 72 Elias Maguli anafunga bao la kufutia machozi kwa njia ya penalti baada ya mchezaji wa Yanga kumchezea rafu ndani ya 18.
Kwa matokeo hayo Yanga wamecheza mechi 27 na kufikisha pointi 68 na kubakiwa michezo 3 huku wakiwa wanahitaji pointi 4 ambazo zitawafanya wachukue ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na ligi hiyo inaendelea leo kwa mchezo moja katika uwanja wa Chamazi Complex matajiri wa jiji la Dar es salaam watawaalika JKT Ruvu walio katika nafasi ya kushuka daraja.
Post a Comment
Powered by Blogger.