Soma Hii Makala Inayozungumzia Jinsi Ya Kuepuka Roho Mbaya.

JINSI YA KUEPUKA ROHO MBAYA
Ni kama kituko, kichekesho au utani kuzungumzia jinsi ya kuepuka kuwa na roho mbaya, wengine wanaiita roho ya korosho au vyovyote vile unavyoweza kuiita.
Hii ni hali ya chuki anayojenga mtu moyoni mwake dhidi ya mafanikio, hatima au uwezo wa mttu mwingine. Hupendi kuona mtu mwingine anakuzidi au anafanikiwa.
Haya ni maradhi anayokuwa nayo mtu tena wakati mwingine hapendi iwe hvy lakini hujikuta tu tayari anachukia hatua yoyote ya mafanikio au maendeleo ya mtu mwingine.
Madhara ya tabia hii ni kuwa mtumwa wa maisha ya wengine, msongo wa mawazo kila uonapo mafanikio ya wengine, kutoweza kupanga mipango halisi kwa maisha yako na mbaya zaidi ni kuishi maisha yasiyo na furaha ktk maisha yako. 


HATUA ZA KUEPUKA
* Jifunze kukubali na kuamini uwezo wa wengine
* Amini kuwa unahitaji watu wengine ili kufikia kilele cha mafanikio
* Elewa, kubali na kuamini kuwa ukiwa duniani wapo wengi watakaokuzidi kwa kipato, ufahamu, uzoefu nk
* Usiruhusu tamaa ikuendeshe bali uitumie kufikia malengo ktk njia sahihi na zinazokubalika
* Jitahidi kuwa wewe wala usitamani uwe mwingine
* Usipende kuishi kwa mashindano bali kwa malengo
* Tumia uzoefu wa waliokuzidi kama somo la kufikia mafanikio yako
* Usiwe mwepesi wa kuangalia udhaifu na mapungufu na kuyashabikia badala ya kuwa mtu wa kujifunza
KUMBUKA: vita kali kuliko zote ni vita dhidi ya nafsi yako mwenyewe hvy jizoeze kufuata Neno la Mungu ili kushinda vita hii na kuishi maisha ya amani siku zote

Post a Comment
Powered by Blogger.