'SINGO' TAMU YA MAREHEMU MWALUVANDA KATIKA ALBUM BORA YA PLUIJM.

Kocha Wa Yanga Pluijm na Msaidizi Wake Mwambusi.
'SINGO' TAMU YA MAREHEMU MWALUVANDA KATIKA ALBUM BORA YA PLUIJM.
Sishangazwi na mafanikio ya Yanga wanayopata kwa kutawala soka la ndani, Sijaona ajabu kwa kikosi hiki kubeba ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na mechi 3 mkononi, hata wakibeba kombe la shirikisho nchini mei 25 kwa kuifunga Azam FC katika fainali kwangu bado haitakuwa habari kubwa.
Naizungumzia Yanga ya kocha mtaalam na mzoefu wa soka la Afrika Hans Van Pluijm akisaidiwa na Juma Mwambusi, hii ni Yanga inayoendeshwa kisomi mno chini ya uongozi wa Yussuf Mehbub Manji.Yanga hii kubeba vikombe vya ndani sio habari ya kushtua, Azam FC wanaopepesuka ama Simba SC walio ICU wataizuia vipi Yanga hii iliyotimia kila idara?kwa ubora huu wa Yanga inapaswa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania, huko ndiko habari kubwa, kushtua na za kusisimua tutazipata____ Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya TP Mazembe kule Lubumbashi, Etoile Sportive du sahel kuiombea Yanga ambaye ni kinara wa kundi A afungwe zaidi ya magoli 7 katika uwanja wa Taifa dhidi ya Mo Bejaia ili watunisia hao watinge nusu fainali, hizi ndizo habari za kusisimua ambazo Hans Van Pluijm anataraji kutuletea, mechi zetu zitarushwa na Supersport huku Thomas Mlambo ama Terry Mbe wakiyataja majina ya Kamusoko, Mwashiuya kwa lafudhi ya kiingereza yenye kubabaika.

Matokeo ya jana katika uwanja wa Estadio Sagrada Esperanca Dundo kwa Yanga kufuzu hatua ya makundi kuna baadhi ya watanzania hawajapendezwa nayo, Yanga imepigana ki-yatima huku wakijua kuna watu wanaikandamiza maksudi!hawa ni wale watu waliotaka ubora wa Yanga usionekane kimataifa. . .
 Baada ya mchezo dhidi ya Yanga hapa Dar, Grupo Desportivo Sagrada Esperanca walipewa muda wa kujiandaa ambapo walicheza mchezo mmoja tu huko kwao, shirikisho la mpira wa miguu nchini Angola likahairisha mchezo wa klabu hiyo dhidi ya Recreativo da Ceala uliopaswa kucheza jumamosi ( 14,May) hii yote kuwaandalia mazingira mazuri mshiriki wake.
Hali ilikuwa tofauti Tanzania, Yanga waliokuwa wanalalamika ugumu wa ratiba waliendelea kulazimishwa kucheza katika viwanja tofauti kama mbio za mwenge kitaifa,kuna wengine walifikia hatua kushtaki kwa waziri mwenye dhamana ya kuendesha michezo nchini Mh. Nape Nnauye wakitaka Yanga wamalize viporo vyao, Yanga walijaribu kukata rufaa hata hivyo shauri lao likatupwa hakukuwa na namna Yanga ikabidi wacheze wakilazimika kutumia usafiri wa anga ili kuepusha uchovu kwa wachezaji wake (tar 10, may) Yanga walikuwa Mbeya dhidi ya Mbeya City, ratiba ikionesha (13, May) wana mchezo dhidi ya Ndanda katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kisha warudi Dar ndipo waende kucheza dhidi ya GD Sagrada Esperanca (18 May ) katika mji wa Dundo kaskazini mwa Luanda takribani Km 1300,
 TFF haikujali wala wenye dhamana ya mchezo huu pia hawakujali, uongozi wa Yanga ulipoona jahazi linazama ukaomba msaada Ndanda mchezo huo ufanyikie Dar, ombi ambalo lilikubaliwa ndipo mchezo ukafanyika jumamosi (14 May) watu wasioitakia mema Yanga ndipo wakaanza kupinga uhalali wa mchezo huo kuhamishiwa Dar, wacha- Mbuzi wa michezo na waandishi uchwara wakashika kalamu zao na kuanza kuponda kitendo hicho cha kizalendo na maslahi kilichofanywa na viongozi wa Ndanda____ hatimaye Yanga wakaondoka kuelekea Angola alfajiri (16 May), huko ilikuwa vita sio mpira tena!kwa ubora wa timu yetu tumeshinda (Ahsante Mungu), sijasahau Nape alipowaagiza Yanga wafanye uchaguzi mkuu wa viongozi wa klabu hiyo mwezi April akitoa takribani wiki 2 tu zoezi hilo kukamilika siku chache kabla ya kuwavaa Al Ahly____ hakuna aliyejali kuwa mafanikio Yanga yatawafaidisha TFF kwa kupewa pesa, ama idadi ya klabu za Tanzania katika michuano ya CAF itaongezwa kutoka mbili hadi tatu pia kuwa nchi yetu inatangazwa na kuletewa sifa,au wachezaji wazawa uzoefu wanaoupata utasaidia kuimarisha timu ya Taifa, ilikuwa vita dhidi ya TFF ambao walishindwa kutuandalia mazingira mazuri Yanga kama mshiriki wake kimataifa, vita dhidi ya wote wenye dhamana ya mpira wa mguu, mwisho wa siku tumeshinda Ubingwa wa ligi kuu, tumefuzu robo fainali kombe la shirikisho barani Afrika pia tupo fainali ya kombe la shirikisho nchini, aibu yetu ama aibu yao??.
Pluijm amenikumbusha mwaka 1998 hii ni baada ya hapo jana kupiga wimbo wa marehemu Tito Mwaluvanda (Pumzika kwa amani)___ Marehemu Mwaluvanda alipewa timu akiwa hana umaarufu wowote ambapo mwenyekiti wa Yanga wakati huo marehem Rashid Ngozoma Matunda alimtambulisha mbele ya wanachama kama msimamizi wa mazoezi huku timu ikiendelea kusaka mwalim wa uhakika, cha ajabu Mwaluvanda akaiwezesha klabu ya Yanga kuchukua ubingwa wa ligi kuu, Kombe la Muungano na kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi klabu bingwa Afrika rekodi ambayo haikuweza kufikiwa na kocha yeyote kabla na baada ikiwa takribani miaka 18 sasa, hata hivyo Mwaluvanda na msaidizi wake Fredy Felix Minziro.
Waliondolewa kwa kigezo hawana uwezo wa kuifundisha timu katika hatua ngumu ya makundi klabu bingwa ndipo wakaletwa Raoul Jean Pierre Shungu, aliyekuwa anasaidiwa na Abeid Mziba 'Tekero', Tayari Hans Van Pluijm ana ngao ya jamii, Ubingwa wa ligi kuu, yupo fainali ya kombe la shirikisho nchini kabla ya hapo jana kutukumbusha wimbo mtamu wa Tito Mwaluvanda katika album yake.

Waambieni wale walioponda mapokezi pale Dida alipobebwa Airport baada ya Yanga kutolewa dhidi ya Al Ahly tulikuwa na maana yetu, mapokezi yale yaliwapa deni vijana wetu na jana wamelipa!nakukumbusha kama ulikuwa na mpango wa kuuza decorder yako ya Dstv usifanye hivyo bali ilipie ili uweze kuishuhudia timu yako_____ Timu yetu leo italala Afrika Kusini itawasili mchana saa nane hapo kesho.


Nakutakia siku Njema Mwananchi.
Admini Hissan Salum Iddi.
Post a Comment
Powered by Blogger.