Simba Yaikimbia Dar es Salaam Kisa Mwadui Ya Julio Jumapili Hii.

Simba.
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea wikendi ili kuhakikisha timu ya Simba inafanya vizuri kwa mechi zake zilizobaki imeamua kulikimbia jiji la Dar es salaam na kujichimbia Visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Matajiri wa madini timu ya Mwadui.

Kikosi hicho kilitua jana visiwani humo kikiwa na wachezaji wote akiwemo na beki Abd Banda aliyekuwa amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu tayari kabisa ya vita dhidi ya kocha msaidizi wa zamani wa Simba Jamhuri Kihwelu Julio ambapo sasa ni kocha mkuu wa Mwadui.
Mwadui Fc.
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili badala Jumamosi amabapo kutakuwa na pambano la shirikisho kwenye uwanja huu wa Taifa swali Julio atakubali kufungwa na Simba.
Post a Comment
Powered by Blogger.