Ripoti Ya WHO,Inasema Umri Wa Kuishi Afrika Umeongezeka Kwa Kasi Ya Ajabu.


Umri wa kuishi barani Afrika unaongezeka kwa haraka ikiwa ni maradufu sawa na maeneo mengine duniani kulingana na shirika la afya dunia WHO.
Ripoti ya WHO inasema tangu mwaka 2000, umri wa kuishi umeongezeka kwa takriban miaka 10 zaidi.Kwa sasa mtu wa wastani anaweza kuishi hadi miaka 60.
Lakini Umri huo bado ni miaka 20 chini ya mtoto anayezaliwa katika mojawapo ya mataifa 29 yenye mapato makubwa.
Daktari Ties Boerma kutoka WHO ameimbia Newsday kwamba sababu moja ni kupungua kwa vifo miongoni mwa watoto inayofanywa na chanjo.
Haya hapa mataifa yenye viwango vya juu vya umri wa kuishi Afrika:
Algeria - 75.6
Tunisia - 75.3
Mauritius - 74.6
Morocco - 74.3
Cape Verde - 73.3
Seychelles - 73.2
Libya - 72.7
Egypt - 70.9
Sao Tome - 67.5
Senegal - 66.7
Taifa la Ethiopia ni la 16 katika orodha hiyo likiwa na kiwango cha kuishi cha wastani wa miaka 64.8,Kenya ikiwa ya 22 na miaka 63.4,Ghana iko katika nafasi ya 25 ikiwa na miaka 62.4,Somalia ni ya 47 ikiwa na miaka 55 na Nigeria ni ya 48 ikiwa na miaka 54.5.
Post a Comment
Powered by Blogger.