Rais Wa Uturuki Asema Bunge Lake Litaweka Vikwazo EU.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema bunge la nchi yake litaweka kikwazo kwenye makubaliano waliyoafikiana na umoja wa ulaya dhidi ya kuzuia mtiririko wahamiaji katika Bahari ya Aegean ,hii ni mbali na bahari ya Mediterranean, bahari ya Aegean iko kati ya Ugiriki na Uturuki ,na kusema kwamba badala yake kuwe na muendelezo wa visa huria kwa wananchi wa Kituruki.
Erdogan pia amesema kwamba msaada wa fedha ulioahidiwa kuiwezesha Uturuki kukabiliana na wimbi la wakimbizi kutoka Syria bado haujatolewa.chini ya makubaliano hayo ni kuwarejesha wahamiaji Uturuki kutoka Ugiriki,mpango ambao unalenga kasi ya kupunguza idadi wahamiaji wafanyao maamuzi ya kuvuka.
Maofisa wa umoja wa ulaya wamesema kwamba hawatatoa vibali vya ukaazi bure kusafiri kutoka Uturuki mpaka Ankara kwani watalazimika kukutana na masharti yote yaliyowekwa na Umoja ikiwa ni pamoja na kurekebisha sheria ya kupambana na ugaidi .
Post a Comment
Powered by Blogger.