Rais Magufuli Kaamua Haya Kuhusu Dkt. Asha Rose Migiro


 Dkt Asha-Rose Migiro ameteuliwa kuwa balozi Wa Uingereza   atachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw Peter Kallaghe ambaye amerejea nyumbani.
Anatarajiwa kuapishwa Alhamisi katika ikulu ndogo ya rais Dodoma.
 Dkt Asha-Rose Migiro aliwahi kufanya kazi kama kama Waziri wa Katiba na Sheria serikali iliyopita na alikuwa miongoni mwa wagombea watatu waliokuwa wamesalia kwenye kinyang'anyiro cha kuteua mgombea wa CCM uchaguzi wa mwaka jana, kabla ya mwishowe Dkt John Magufuli kuidhinishwa. 
 Dkt. Asha Migiro pia aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa.
Post a Comment
Powered by Blogger.