Rais Magufuli Ataja Wizara Inayoongoza Kuwa Na Watumishi Hewa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Rais Dkt John Magufuli amesema Ofisi ya Waziri Mkuu  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inaongoza kwa kuwa na watumishi hewa  8,373 ikifuatiwa na Serikali Kuu ambayo ina 1,922.
  Kauli hiyo aliitoa Jana mjini Dodoma alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi  kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani inayofanyika Mei 1kila mwaka.

Rais John Magufuli.

  Alisema wafanyakazi hewa wameigharimu serikali fedha Nyingi ambazo zingeweza kuboresha maslahi ya wafanyakazi halali na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema hadi sasa wafanyakazi hewa nchi nzima ni 10,295 na wamekuwa mshahara kila mwezi sh.bilioni 11,603,273,799.41 kila mwezi huku sh.bilion 139, 239,285,592.92 zikilipwa kila mwaka na zikizidishwa kwa miaka mitano zinakuwa sh.bilioni 696,196,427,964.6.

Mh.Magufuli.
Rais aliongeza kuwa fedha hizo zingeweza kutumika katika kufanya vitu vingi ikiwemo miundombinu ya afya na elimu pamoja na kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
Post a Comment
Powered by Blogger.