Rais Jacob Zuma Asubiri Uamuzi Kuhusu Mashtaka Leo.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Waendesha mashtaka mkuu nchini Afrika Kusini wanatarajiwa kufichua leo iwapo watafufua mamia ya mashtaka ya ulaji rushwa dhidi ya Rais Jacob Zuma au la.
Hii ni kufuatia uamuzi wa mahakama mwezi jana ambayo ilisema uamuzi wa kutupilia mbali mashtaka hayo haukuwa wa busara na unafaa kutafakariwa upya.
Mashtaka hayo yanajumuisha kashfa kubwa ya mabilioni ya dola ya ununuzi wa silaha iliyofutiliwa mbali mwaka 2009.
Kufutiliwa mbali kwa mashtaka hayo kulimfungulia njia Bw Zuma kushinda urais wiki chache baadaye.
Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanasema iwapo mashtaka hayo yatafufuliwa, basi hatua hiyo itaongoeza shinikizo za kumtaka Bw Zuma ajiuzulu.
Post a Comment
Powered by Blogger.