Picha Ya Justin Bieber Akitoa Busu Kwa Mpenzi Wake Selena Gomez Lilivyovutia Instagram.


Picha ya mwanamuziki Justin Bieber akimpiga busu aliyekuwa mpenziwe Selena Gomez ndio picha iliopendwa na wengi katika mtandao wa instagram.
Imependwa na watu milioni 3,569,000 huku watu 350,000 wakiipenda dakika 15 tu baada ya kuchapishwa.
Picha hiyo iliokuwa na maelezo chini yake yalioandikwa ''Feels'' imeipiku picha ya Kendal Jenner ambayo ndio picha iliopendwa sana huku nayo ikizungumziwa karibu mara milioni.
Picha ya nywele zake ilishinda mwaka 2015 na hivyo basi kuishinda picha ya dadaake Kim Kardashian ya harusi na Kanye West mwaka 2014.
Selena na Justin waliachana mwaka 2014 lakini mtandao haujamalizana na ''Jelena''.
Pia Bi Gomez aliipenda baada ya Justin Bieber kuichapisha.Justin Bieber sasa ana takriban wafuasi milioni 70 katika mtandao wa Instagram.
Picha yake ya hivi majuzi akimshika chui milia imependwa mara milioni mbili lakini haikuishinda picha ya Bieber aliyokifua wazi ambayo imependwa mara milioni 2.2.

Post a Comment
Powered by Blogger.