Paul Makonda Atangaza Neema Kwa Watumishi Wa Serikalini Wanaoishi Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameahidi kuwajengea nyumba za kuishi watumishi wa serikali waliopo mkoani kwake ili waondokane na kero za kodi ya nyumba.
Makonda aliyasema hayo Jana katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika jijini Dar es salaam.

Paul Makonda.

  Alisema watumishi wamekuwa wakipata tabu Nyingi kutokana na mishahara kutokukidhi mahitaji ya maisha huku akisisitiza kuwa mishahara hiyo haitoshi kuhimili mazingira ya jiji la Dar es salaam.

Mh.Makonda.
Alisema tayari wameanza kutengeneza baadhi ya ramani ambazo wafanyakazi hao watachagua wanazozitaka Aliongeza kuwa katika hatua za uboreshaji wa mazingira ya kufanyia kazi wameanza na walimu ambao ni kundi kubwa kwa kuwawezesha kusafiri bure.
Post a Comment
Powered by Blogger.